Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa kwenye Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Bandaranaike, mjini Colombo Sri Lanka na Mheshimiwa
Chandrasiri Gajadeera, Waziri wa Rehabilitation and Reforms wan chi
hiyo wakati alipowasili leo asubuhi kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa
Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Madola unaoanza tarehe 15.11.2013.PICHA NA JOHN LUKUWI
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Waziri wa Rehabilitation and
Reforms wa Sri Lanka Bwana Chandrasiri Gajadeera, mara baada ya
kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bandaranaike huko
Colombo, mji mkuu wan chi hiyo tarehe 14.11.2013. Mama Salma amefuatana
na Rais Kikwete kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Madola .
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiambatana na Mkewe Mama Salma akitia saini kwenye
kitabu cha wageni mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa
Bandaranaike nchini Sri Lanka kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi za
Jumuia ya Madola tarehe 14.11.2013.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu maalumu cha Wageni muda mfupi
baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Colombo nchini
Srilanka kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Madola
Commonwealth unaofanyika nchini Srilanka(Picha na Freddy Maro)
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakilakiwa kwa
ngoma za kitamaduni mara baada ya kuwasili jijini Colombo, Sri Lanka,
leo Novemba 14, 2013 tayari kwa mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya
madola (CHOGM)
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiongea na
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue mara baada ya kuwasili jijini
Colombo, Sri Lanka, leo Novemba 14, 2013 tayari kwa mkutano wa wakuu wa
nchi za jumuiya ya madola (CHOGM
PICHA NA IKULU 2013).
Post a Comment