WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – AJALI YA MOTO.
MNAMO TAREHE 09.11.2013 MAJIRA YA SAA 21:00HRS HUKO MLIMA RELI, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA UTENGULE –USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA, FROLA D/O KYENGE, MIAKA 33, KYUSA, MHUDUMU WA BAR ,MKAZI WA MLIMA RELI ALITOA TAARIFA YA KUUNGUA MOTO NYUMBA ANAYOISHI NA KUTEKETEZA MALI ZOTE ZILIZOKUWA NDANI YA NYUMBA HIYO. NYUMBA ILIKUWA NA VYUMBA VITANO WANAVYOISHI WAPANGAJI WATANO TOFAUTI, IMEJENGWA KWA MATOFALI YA KUCHOMA NA KUEZEKWA BATI MALI YA JOHN S/O PONDAMALI MKAZI WA DSM. CHANZO KINACHUNGUZWA. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA BADO KUFAHAMIKA NA HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA, UPELELEZI WA TUKIO HILI UNAENDELEA.
WILAYA YA MBOZI – WIZI WA MIFUGO.
MNAMO TAREHE 08.11.2013 MAJIRA YA
SAA 23:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA BARA, KATA YA BARA, TARAFA YA
IGAMBA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. SIMITON S/O KABURU, MIAKA 36,
MNYIHA, MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA BARA ALIGUNDUA KUIBWA KWA
MIFUGO[NG’OMBE] WAKE KUMI NA TATU[13] WENYE THAMANI YA TSHS 6,000,000/=
NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. MBINU NI KUVUNJA ZIZI. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTU/WATU WALIOHUSIKA NA
TUKIO HILI PAMOJA NA NG’OMBE WALIOIBWA ATOE TAARIFA KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE MARA MOJA.
WILAYA YA CHUNYA – AJALI YA GARI KUPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 09.11.2013 MAJIRA YA
SAA 18:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHALANGWA, KATA YA CHALANGWA,
TARAFA YA KIWANJA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. GARI T.672 ASF AINA
YA TOYOTA PRADO MALI YA KAMPUNI YA UJENZI YA CHINESE COMMUNICATION
& CONSTRUCTION LTD LIKIENDESHWA NA DEREVA AZIZ S/O ABDALAH, MIAKA
30, MUHA, FUNDI MAGARI WA KAMPUNI HIYO, MKAZI WA CHALANGWA LILIPINDUKA
NA KUSABABISHA KIFO CHA DEREVA HUYO PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI KWA KUZINGATIA SHERIA NA
ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI- ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Post a Comment