Mkurugenzi
Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akielezea kwa waandishi
wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam mapema hii leo juu ya
mikakati ya kuinua utalii hifadhi za kusini na magharibi kwa kutenga
maeneo 34 ya uwekezaji, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari
(MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
Baadhi ya
waandish wa Habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi
za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi wakati akielezea mikakati ya kuinua
utalii hifadhi za kusini na magharibi kwa kutenga maeneo 34 ya
uwekezaji.
Picha na Eliphace Marwa, MAELEZO (P.T)
Hifadhi ya Serengeti ni moja kati ya maajabu Saba Barani Afrika.
Hifadhi ya Mikumi inapatikana Mkoa wa Morogoro
Hifadhi za milima Udzungwa inapatikana katika mkoa wa Morogoro ni moja ya vivutio vinavyopatikana nchini Tanzania.
Frank Mvungi-Maelezo
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
limetenga maeneo 34 kwa ajili ya uwekezaji katika huduma za malazi kwa
wageni wanaotembelea Hifadhi za Kusini na Magharibi mwa nchi kwa ajili
ya utalii.Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi mkuu wa TANAPA bw. Allan Kijazi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya shirika hilo kupanua Sekta ya utalii hapa nchini hasa kwa kupanua huduma za malazikatikahifadhizaKilimanjaro,Katavi,Mikumi,Mkomazi,Ruaha,Saadani,tarangire,Rubondo na Kitulo.
Akifafanua zaidi bw. Kijazi alisema lengo la Tanapa ni kuhakikisha kuwa maeneo yaliyotengwa yanapata wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi ambapo kutafanyika kongamano maalum mwezi Februari 2014.
Bw. Kijazi alisema kuwa kongamano hilo litawaleta pamoja wakezaji wakubwa na wadogo ambao watapata fursa ya kuyafahamu maeneo hayo na namna gani uwekezaji wao utakavyoleta faida kwa sekta ya utalii na uchumi nchini.
Aidha Bw. Kijazi alisema kwamba vitanda katika maeneo ya hifadhi kwa sasa kuna vitanda 6,681 ambapo kwa miaka mitano ijayo idadi hii itafikia vitanda 8,421.
Aliweka bayana kuwa uamuzi wa TANAPA kutenga maeneo mapya ya uwekezaji umezingatia ukuaji wa sekta ya utalii nchini ambapo karibu asilimia 75 ya wageni wanaofika nchini ni watalii.
Baadhi ya vivutio vinavyoifanya Tanzania kuongoza katika Afrika na Dunia katika Sekta ya utalii ni pamoja na Hifadhi za Taifa Ruaha,Mahale,Gombe,Katavi,Tarangire.
Vivutio vingine ni Ziwa manyara, Arusha,mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na pori la Akiba la Selous.
Mwisho
Post a Comment