Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Tanesco latangaza mgawo wa umeme

 

 
Katika kile kinachoaminika ni mgawo wa umeme, Shirika Umeme nchini (Tanesco), limetangaza kuwapo kwa upungufu wa umeme nchini kwa siku kumi kuanzia leo.
Meneja Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud, amesema tatizo hilo litaikumba mikoa yote inayotumia umeme wa gridi ya taifa.

Alisema tatizo hilo limetokana na upungufu wa gesi kutoka katika Kisiwa cha Songosongo, wilayani Kilwa, mkoani Lindi unaosababishwa na matengenezo ya kiufundi kwenye visima vya gesi unaofanywa na Kampuni ya Pan Africa.

Badra alisema lengo la matengenezo hayo ni kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo. "Kutokana na matengenezo hayo, mikoa iliyounganishwa katika gridi ya taifa itaathirika kwa kukosa umeme kwa baadhi ya maeneo kwa nyakati tofauti," alisema.

Badra alisema kuwa Tanesco imepokea barua kutoka Kampuni ya Pan Afrika inayowajulisha kuzimwa kwa mitambo ya gesi kwa ajili ya kupisha matengenezo ya kiufundi kwenye visima hivyo kuanzia leo hadi Novemba 26.


Alisema suala hilo ni la kiufundi ambalo haliwezi kukwepeka, hivyo umeme utakaokuwa ukitumika ni ule utokanao na mafuta na maji yatokanayo na mabwawa.

Alisema Tanesco imeamua kuwekeza nguvu kubwa ya umeme katika gesi na kwamba kwa sasa  mitambo yote inayotumia mafuta kwa ajili ya kuzalisha umeme imepelekewa mafuta ya kutosha.

Alisema katika maeneo nyeti ikiwamo hospitali, Tanesco imejitahidi yasiathirike na upungufu huo wa umeme. Aidha, alisema kutokana na hali hiyo maeneo kadhaa yatalazimika kuwa kwenye mgawo wa umeme  kwa saa chache.

Aliitaja mikoa ambayo haitaathirika kuwa ni Lindi, Mtwara, Kagera na Katavi na kwamba mikoa mingine iliyobaki itakabiliwa na tatizo la upungufu wa umeme ikiwamo Zanzibar.

Pia alisema uongozi unaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kwa baadhi ya maeneo yatakayokuwa yakikosa umeme.

CHANZO: NIPASHE
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top