Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Tanzania na China zakubaliana kushirikiana katika masuala ya Serikali za Mitaa


Waziri wa  Nchi  Tawala za Mkoa na Serikali za   Mitaa(TAMISEMI), Hawa Ghasia wakati akizungumza na waaandishi wa habari leo jijini  Dares Salaam kuhusu ujio wa wageni hao, ambao watakuwepo nchini kuanzia Novemba 23 hadi 26, mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mkoa na Serikali za   Mitaa(TAMISEMI),(kushoto ) na   Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa  wakifuatilia mkutano wa   waaandishi wa habari leo jijini  Dares Salaam kuhusu ujio wa wageni hao, ambao watakuwepo nchini kuanzia Novemba 23 hadi 26, mwaka huu.

 Jumla ya wageni 70 kutoka China wanatarajia kufanya ziara nchini Tanzania ili  kudumisha ushirikiano katika masuala  mbalimbali ya Serikali za Mitaa.
 Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa  Nchi  Tawala za Mkoa na Serikali za   Mitaa(TAMISEMI), Hawa Ghasia wakati akizungumza na waaandishi wa habari leo jijini  Dares Salaam kuhusu ujio wa wageni hao, ambao watakuwepo nchini kuanzia Novemba 23 hadi 26, mwaka huu.
 Waziri Ghasia alisema ujumbe huo utakutana na Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na baadhi ya mawaziriwa sekta mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa,, makatibu wakuu tawala wa mikoa, mameya wenyeviti wa halimashauri za jiji, Manispaa, miji na baadhi ya wakuu wa wilaya, wakurugenzi  wa halimashauri hizo.
Aidha ameongeza kuwa kutakuwepo na mkutano mkubwa utakaofanyika Novemba 25 ,mwaka huu   kwenye Ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dares Salaam.
“Lengo la ujio huo ni kuanzisha rasmi ushirikiano kati ya Serikali  za Mitaa za Tanzania na China. Kupitia umoja huo ushirikiano kati ya Serikali za Mitaa za Tanzania na China utakuwa wa kimkakati zaidi. Ili kufanikisha ziara hii Serikali Kuu imewataka  wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi zilizoko chini ya ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kubaini fursa za uwekezaji na kuaanda mipango yao ya kuanzisha miradi ya maendeleo ,”alisema Waziri Ghasia.
 Alisema Tanzania itanufaika katika  katika maeneo ya Uchumi, miundombinu  mfano barabara ,Biashara, Elimu ya Jamii, Sayansi, Teknolojia,Utamaduni na maeneo mengine.
Waziri Ghasia aliongeza kwamba kupitia ushirikiano huo kutakuwepo na utoaji tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri 100 wa shule za msingi na 100 kwa shule za sekondari.Pia kutakuwepo na ziara zaidi za watumishi wa halimashauri hizo.
 
( Picha  na habari na  Magreth Kinabo) 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top