Baadhi
ya Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari ya Malindi Zanzibar
yakisubiri kuhisabiwa kupata idadi kamali na thamani yake na uzito kwa
ujumla.
Kamanda
wa Kikosi cha Polisi Bandarini Zanzibar akiongoza Operesheni wa kukagua
magunia yaliokuwa na Pembe za Tembo yaliokamatwa katika bandari hiyo
jana yakiwa katika harakati ya kusafirishwa nje ya Nchi kupitia bandari
hiyo, zoezi hilo limefanywa chini ya Jeshi la Polisi Bandari Kikosi cha
KMKM, yalikuwa katika Kontena la futi 40.
Askari
wa jeshi la Polisi wakitowa Pembe za Tembo katika makunia wakati wa
zoezi hilo leo asubuhi katika bandari ya Malindi Zanzibar.
Magunia
haya yakiwa na sehena na makombe ya pwani wakati katikati yakiwa na
viroba vya mPembe za Tembo ambayo yakiwa yamehifadhiwa katika Kontena
likiwa tayari kusafirishwa nje ya Nchi, limegunduliwa katika bandari ya
Zanzibar jana asubuhi.
Zoezi likiendelea kupekuwa makunia ya Makombe ya Pwani kutowa magunia yaliohifadhiwa Pembe za Tembo
Operesheni
Ikiendelea kuhesabu Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari ya
Zanzibar wakiweka hesabu sawa kuhakikisha hesabu iliokamilika na kupata
thamani yake halithi.
Zikipimwa uzito kujuwa uzito wake kila gunia likipimwa kupata uzito wake wote. CHANZO: ZANZINEWS
Post a Comment