Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Vigogo hawa kunyang’anywa vitalu vya madini

HATIMAYE serikali imetangaza kuanza kuwanyang’anya vigogo waliojimilikisha vitalu vya uchimbaji wa madini bila kuviendeleza. Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (pichani), wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kukabidhiwa mgodi wa Tulawaka na Kampuni ya African Barrick Gold (ABG).

Profesa Muhongo alisema katika kuhakikisha rasilimali ya madini inawanufaisha Watanzania wote, serikali imeanza mchakato wa kuwanyang’anya vitalu wamiliki wanaoonekana kusuasua kuviendeleza na kuwapatia wachimbaji wadogo.

“Serikali imeanza kusikiliza kilio cha wachimbaji wadogo kwa kutenga maeneo mbalimbali ambayo yatarahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali, ikiwamo kupatiwa mikopo na vifaa,” alisema.


Akizungumzia suala la ununuzi wa mgodi huo, Profesa Muhongo alisema dhamira ya serikali ni kuhakikisha STAMICO inaimarika kwa kuanzisha kampuni mbalimbali.

“STAMICO itachukua mgodi wa dhahabu wa Tulawaka na baadhi ya leseni za utafutaji wa madini zinazozunguka eneo la mgodi kwa gharama ya dola za Marekani milioni 4.5.

“Kama sehemu ya makubaliano hayo, shirika litachukua umiliki na usimamizi wa mfuko wa fedha za ukarabati wa mazingira, ikiwa kama sehemu ya mpango wa ufungaji wa mgodi huo,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Gary Mwakalukwa, alisema kutokana na makubaliano hayo, Watanzania pia wataweza kununua hisa za kampuni hiyo.

“Kwa sababu ndani ya Stamico, tutaunda kampuni ya serikali ya madini itakayoitwa Stamigol, ambayo itashughulikia kusimamia shughuli zote za mgodi huo wa dhahabu,” alisema.

Naye Makamu wa Rais wa ABG, Deo Mwanyika, alisema Tulawaka ulikuwa ni mgodi wenye mafanikio makubwa kwa kampuni hiyo, hivyo makubaliano hayo ya biashara na STAMICO ni fursa ya kuendeleza sekta ya madini nchini.


RAI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top