NYONGEZA YA TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 13. 11. 2013.
WILAYA YA RUNGWE – WATUHUMIWA WANNE WALIOHUSIKA NA
TUKIO LA MAUAJI YA MAREHEMU JOHN
AFWILILE MWANKENJA WAPATIKANA NA HATIA
TUKIO LA MAUAJI YA MAREHEMU JOHN
AFWILILE MWANKENJA WAPATIKANA NA HATIA
MAHAKAMANI.
§ MNAMO
KATI YA TAREHE 12.11.2013 KATIKA KIKAO CHA MAHAKAMA KUU KANDA YA
MBEYA KILICHOFANYIKA TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA,
WATUHUMIWA WATATU 1.AKIMU S/O MSELEM MWAKALINGA , 2. DAUDI S/O JUSTI
MWASIPASA, 3. OBETE S/O MWANYINGILI ANGANISHE MASUNGO NA 4. KELVIN S/O
MAURUS MYOVELA WALIPATIKANA NA HATIA KUFUATIA KUHUSIKA NA TUKIO LA
MAUAJI YA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE
MAREHEMU JOHN AFWILILE MWANKENJA.
§ KATIKA
HUKUMU ILIYOSOMWA NA MHE JAJI S.VJ. KARUA, WATUHUMIWA AKIMU S/O
MSELEM MWAKALINGA NA DAUDI S/O JUSTI MWASIPASA WALIHUKUMIWA HUKUMU YA
KIFO [KUNYONGWA] NA WATUHUMIWA OBETE S/O MWANYINGILI ANGANISHE MASUNGO
NA KELVIN S/O MAURUS MYOVELA WALIHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA SABA [07]
KWA KUSAIDIA KUTENDEKA KWA KOSA.
§ AWALI
MNAMO TAREHE 19.05.2011 MAJIRA YA SAA 20:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
KIWIRA, KATA YA KIWIRA ,WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA, MAREHEMU JOHN
S/O AFWILILE MWANKENJA, MIAKA 50, KYUSA, ALIYEKUWA M/KITI WA
HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE, DIWANI WA KATA YA KIWIRA NA PIA
MWENYEKITI WA CCM WILAYA HIYO AKIWA ANATOKEA MBEYA MJINI NA GARI T.127
ACZ AINA YA NISSAN DOUBLE CABIN ALIPOFIKA ENEO LA NYUMBANI KWAKE
ALIPIGWA RISASI NNE KICHWANI NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO.
§ KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHANA NA UOVU/UHALIFU WA AINA YOYOTE ILE ILI
KUJENGA JAMII NA NCHI ILIYOBORA NA YENYE MAENDELEO.
WILAYA YA RUNGWE – MTUHUMIWA MMOJA APATIKANA NA HATIA KWA KOSA LA
KUBAKA NA KUUA MTOTO MDOGO.
KUBAKA NA KUUA MTOTO MDOGO.
§ MNAMO
TAREHE 12.11.2013 HUKO KATIKA KIKAO CHA MAHAKAMA KUU KANDA YA MBEYA
KILICHOFANYIKA TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA, MTUHUMIWA
BARAKA S/O JAILO MWANDEMBO,MIAKA 34,KYUSA, MFANYABIASHARA, MKAZI WA
BULYAGA – TUKUYU ALIPATIKANA NA HATIA KUFUATIA KUHUSIKA NA TUKIO LA
MAUAJI YA MTOTO MDOGO MWENYE MIAKA MITANO.
§ AWALI
MNAMO TAREHE 21.01.2010 MAJIRA YA SAA 17:00HRS MTUHUMIWA ALIONEKANA
AKIONGEA NA MTOTO HUYO NA KISHA MTOTO KUPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA
KUTATANISHA. WANANCHI KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI WAKIWA KATIKA
MSAKO WA KUMTAFUTA MTOTO HUYO TAREHE 22.01.2012 MAJIRA YA SAA 00:30HRS
MAREHEMU ALIKUTWA KICHAKANI AKIWA HANA JERAHA UMBALI WA KILOMITA 1
KUTOKA NYUMBANI KWAO AKIWA AMEBAKWA KISHA KUUAWA.
§ KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA UOVU/UHALIFU WA AINA YOYOTE ILE
ILI KUJENGA JAMII ILIYOBORA NA YENYE MAENDELEO.
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment