Mwenyekiti wa Tume ya Katiba,Jaji Joseph Sinde Warioba akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kukabidhi kwa Rais,Rasimu ya Pili ya Katiba iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee,jijini Dar es Salaam.Jaji Warioba alisema kuwa kulingana na idadi ya kura zilizopatikana kutoka kwa wananchi kuhusu uundwaji wa Serikali tatu, alisema kuwa idadi kubwa zaidi ni ya watu waliohitaji Serikali tatu kuliko walioipinga, hivyo Serikali tatu haipingiki ambapo kwa sasa itabaki ni kazi ya maamuzi ya Bunge la Katiba linalotarajia kuundwa mapema mwezi Januari mwakani.
Rasimu ya Katiba hii ni ndefu kuliko ya kwanza ina ibara 271 ya kwanza ilikuwa na ibara 240
-wananchi wametoa maoni mazito kuhusu uongozi na utawala bora
-lugha ya kiswahili lugha ya taifa.
-Madaraka ya Rais yamepunguzwa.
-wabunge wasiwe mawaziri
-kuwe na ukomo wa wabunge
-wananchi wawajibishe wabunge
-spika/naibu wasiwe wabunge wala viongozi wa juu wa vyama vya siasa.
-kuwepo na jeshi moja la Polisi na Usalama wa Taifa.
MUUNGANO
39000 walitoa maoni kuhusu muungano Tanzania Bara,na karibu wote wa Zanzibar walitoa maoni kuhusu muungano
-Taasisi nyingi zilipendekeza serikali tatu.
Malalamiko upande wa zanzibar
Serikali ya Tanganyika imevaa koti la Tanzania
-mambo ya muungano yamekuwa yakiongezeka
-kumuondoa rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais
Malalamiko Tanzania Bara.
-Zanzibar imebadili katiba yake na kuchukua madaraka ya Jamuhuri ya Muungano
-Wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar
Mambo mengi ya Muungano yamebadilishwa bila kufuata Katiba.
TUME IMEPENDEKEZA MUUNDO WA MUUNGANO UWE WA SERIKALI TATU
Post a Comment