Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akitia saini kitabu cha
maombolezo ya Kifo cha Mpigania Uhuru wa Afrika kusini Rais wa Kwanza wa
Taifa hilo Mzee Nelson Mandela hapo katika Ubalozi wa Nchini Mtaa wa
Masaki Jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimpa pole Balozi wa Afrika ya
Kusini Nchini Tanzania Balozi Thanduyise Chiliza kufuatia kifo cha Rais
mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kilichotokea mwishoni mwa
wiki iliyopita.
Katibu
Mkuu wa CCM Nd. Abdullrahman Kinana akimshindikiza Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julus Nyerere Jijini Dar es salaam akielekea Nchini
Afrika Kusini kuhudhuria Sala Maalum ya kuuaga mwili wa Kiongozi
mashuhuri Duniani Rais wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiagana na Katibu Mkuu wa CCM
Nd. Abdullrahmana Kinana tayari kupanda ndege kuelekea Nchini Afrika
Kusini. Nyuma yake Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi.(Picha
na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ).
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameondoka Nchini leo
jioni kuelekea Johannesburg Afrika ya Kusini kwa ajili ya kuhudhuria
sala Maalum ya pamoja ya kuuaga mwili wa Kiongozi mashuhuri Duniani Rais
Mstaafu wa nchi hiyo Mzee Nelson Mandela.
Sala
hiyo maalum inayotarajiwa kufanyika kesho kwenye uwanja maarufu wa NFP
nchini Afrika Kusini inatarajiwa kuhudhuria na Viongozi kutoka zaidi ya
nchi sabini Ulimwenguni.
Kwenye
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es
salaam Balozi Seif aliagwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Nd.
Abdullrahman Kinana pamoja na baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na Serikali
zote mbili za SMT na SMZ.
Balozi
Seif aliyefuatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi akimuwakilisha Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein
ni miongoni mwa Ujumbe wa Tanzania utaoshiriki tukio hilo ukiongozwa na
Rais wa Jamuhuri yaMuungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar anatarajiwa kurejea Zanzibar kesho kutwa jioni ya Tarehe 11 mwezi Novemba mwaka 2013.
Marehemu
Mzee Nelson Madela anayetarajiwa kuzikwa Jumapili ijayo alikuwa
Kiongozi shupavu wa Afrika Kusini aliyesimama imara kuongoz mapambano
dhidi ya ubaguzi wa rangi uliokuwa ukiendeshwa na Makaburu waliyokuwa
wakiitawala nchi hiyo.
Harakati
hizo za Mzee Mandela zilipata nguvu kutokana na msaada wa baadhi ya
viongozi kadhaa Barani Afrika ambazo hatimaye Makaburu hao wakaamua
kumfungulia mashtaka na kufungwa jela kwa takriban miaka 27 katika
Kisiwa cha Robin ambacho sasa kimekuwa sehemu kubwa ya Utalii Nchini
Afrika Kusini.
Kiongozi
huyu ambae ni wa aina yake hapa Duniani alisimama imara kudai haki za
watu weusi waliokuwa wakinyanyaswa na kukandamizwa kwa sababu tu ya
rangi yao.
Post a Comment