Bomu
ambalo liliokotwa na mwanafuzni wa kidato cha tatu shule ya sekondari
Mji Mpya Emmanuel Stanley jirani na kambi hiyo ya zamni ya wakimbi wa
Afrika kusini..
Mwanafunzi
wa kidato cha tatu shule ya Sekondari ya Kata ya Mji Mpya Emmanuel
Stanley[17] ameokota bomu viwanja vya kanisa maombi na maombezi
lililopo eneo la Barakuda Kata ya Mazimbu manispaa ya Morogoro jirani na
iliyokuwa kambi ya wakimbizi wa Afrika Kusini.
Bila
kujua kama hilo ni bomu mwanafunzi huyo alianza kulicheza kabla ya
mwenzake aliyefahamika kwa jina moja la Evon kumshtua kwamba hilo ni
bomu ambapo kwa pamoja wanafunzi hao walitoa taarifa kwa wazazi wao
ambao nao walitoa taaria kwa serikali ya mtaa huo
Geti kuu
la kuingia campus ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine[SUA] ambayo
zamani ilikuwa kambi ya Wapigania uhuru wa Afrika Kusini
CHANZO : MATUKIO BLOG
Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa Bw Kaloli Joseph Poul akimuoneysha bomu hilo
Akihojiwa
na mwandishi wetu mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Modeko 'B' Bw
Kaloli Joseph Poul amethibitisha kuwepo kwa bomu hilo katika mtaa wake
na kudai.
"
Nikweli kama unavyoliona bomu hili limeokotwa na mwanafunzi Emmanuel
kwenye eneo hili la kanisa,awari mwanafunzi huyo hakugundua kama ni
bomu ambapo alilichezea kwa muda kabla ya mwenzake aliyefahamika kwa
jina moja la Evon kumstua kwamba hilo ni bomu kwa pamoja watoto hao
walitoa taarifa kwa wazazi ambao nao walitujulisha sisi viongozi wa mtaa
na kwamba nasisi tuli ripoti tukio hilo Polisi"alisema mwenyekiti huyo
na kuendela kusema.
"Kundi
la mapolisi 12 waliojaa kwenye Difenda mbili walifika eneo hilo na
tukio na kuthibitisha kwamba hilo ni bomu ambapo nao waliwaita wanajeshi
wa kikosi cha Mzinga ambao baada ya kufika walidaikwamba bomu hilo ni
la muda mrefu na kwamba linaweza kulipuka wakati wowote hivyo kwa muda
huu wamekwenda kambini kwao kuchukua vifaa kwa lengo la kuja kulilipua
hapa hapa na kwamba wamedai kwamba wakati shughuri hiyo ya kulipua bomu
hilo ikifanyika wananchi wote wanatakiwa kuondoka katika mtaa huu
umbali wa mita 400 na sisi kama viongozi wa mtaa tayari tumeshawatangazi
wananachi wetu na kwamba kwa sasa eneo hili lina lindwa na
polisi"alisema kiongozi huyo wa mtaa
Kwa
upande wake mchungaji wa kanisa hilo Bi,Tabia Mwalusako alipohojiwa na
mwandishi wetu alisema anamshukuru Mungu kwa kuendelea kuwalita na
tukio hilo la hatari
"
Tukio hili limetustua sana lakini mungu wetu ambaye ni Mlinzi wa maisha
yetu ametulinda hebu fikiria watoto wale waliliokota bomu lile na
kulichezea kwa dakika kadhaa bila kuwazulu pia nitumia fursa hii
kukanusha habari zilizozagaa mjini kwamba tukio hili linahusihwa na
ugaidi wazee wa eneo hili walisema kwamba campus hii ya SUA awari
ilikuwa akikaliwa na wakimbi wa Afrika kusini hivyo bomu kuonekana eneo
hili sio jabo la ajabu zaidi ya yote bomu hili lilifukiwa muda mrefu
ardhin kabla ya kuokotwa na hawa watoto waliokuwa wakilima kwenye bustan
hii"alisema Mchungaji huyo.
Post a Comment