DUA maalum ya kumbukumbu na kumuombea aliyekuwa msanii wa filamu Bongo, Marehemu Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ imezua minong’ono mingi kufuatia wasanii wengi wanaounda Kundi la Bongo Movie kudaiwa kumfanyia mbaya mkewe, Wastara Juma kwa kutohudhuria, Ijumaa Wikienda lilikuwepo.
Dua hiyo ya ilifanyika Jumamosi iliyopita nyumbani kwa marehemu Tabata-Bima, Dar na kumalizikia kaburini kwake Kisutu.
Katika tukio hilo, wadau mbalimbali wa filamu na burudani, walionekana kushangazwa na kitendo cha wasanii wengi wa Bongo Movie kutokuwepo licha ya marehemu Sajuki kushirikiana nao kwa karibu enzi za uhai wake.
Aidha, wengine walifika mbali kwa kuhoji kulikoni wafanye hivyo, maswali ambayo yalimuongezea uchungu mkubwa Wastara aliyekuwa akibubujikwa machozi mara kwa mara.
Kwa upande wake, Wastara alisema anamshukuru Mungu kwa kufanikisha shughuli hiyo na kuwaombea kwa Mungu wote waliojitokeza kumuunga mkono kwenye dua hiyo.
“Nawashukuru wote waliojitokeza, wamenifariji sana,” alisema Wastara kwa simanzi.
Wasanii wa filamu waliohudhuria dua hiyo, ni pamoja na Denis Sweya ‘Dino’, Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Flora Mvungi, Hamis Ramadhan ‘H. Baba’ na Suleiman Bin Sinan ‘Bond’.
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Vincent Kigosi ‘Ray’ alipotafutwa, simu iliita bila kupokelewa.
Sajuki alifariki dunia Januari 2, 2012 na katika kutimiza mwaka mmoja kaburini misa nyingine itafanyika nyumbani kwa wazazi wake mkoani Songea Januari 2, 2014.
GPL
Post a Comment