Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BREAKING NEWSSSS ... Basi la Simiyu Express laua wawili na 14 hoi hospitalini

WATU wawili wamekufa na wengine 14 kujeruhiwa baada ya basi waliolokuwa
wakisafiria la Simiyu Express kupinduka katika eneo la Ihumwa nje kidogo ya
manispaa ya Dodoma.

Basi hilo lenye namba za usajili T 717 ANL aina ya scania basi lilikuwa
likiendeshwa na dereva aliyetambulika kwa jina la Mramba Issa (31).

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kaimu Kamanda wa Polisi
mkoani hapa Susan Kaganda, alisema kuwa basi hilo lilikuwa linatokea
Bariadi kwenda Dar es salaam likiwa na abiria 60 liliacha njia na kupinduka
kutokana na mwendo kasi .

Kamanda alisema kwamba ajali hiyo ilitokea leo alfajiri majira ya saa tisa
usiku katika barabara ya Dodoma-Dar es salaam  eneo la Elshadai .

Kamanda Kaganda aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni pamoja na
dereva wa basi hilo Mramba Issa mkazi wa Magomeni Dar es salaam na Frola
Erenest(21) Mwali wa shule ya msingi Mwamoto kolokolo, Bariadi.

Aidha kamanda akizungumzia zaidi ajali hiyo alisema kwamba basi hilo
lilikuwa likiwakwepa askari wa barabarani kwa kupita njia za panya.
Alifafanua kuwa kwa basi hilo kusafiri usiku huo ni kukwepa askari .

Aliwataka pia wamiliki wa magari kuweka madereva wawili kwa magari ya
masafa marefu na pia wazingatie sheria za barabarani.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top