Kepteni wa timu ya Jumuiya ya Afrika akinyanyua Kombe la Mshindi wa tatu katika Netiboli.
Rais
Yoeri Kaguta Museveni akipiga danadana kabla ya pambano la Soka la
fainali kati ya timu ya Bunge la Uganda na timu ya Bunge la Jumuiya ya
Afrika Mashariki ambapo Uganda imeshinda kwa 3-0.
Kepteni
wa timu ya Netiboli ya Bunge la Tanzania Grace Kihwelu akinyanyua kombe
juu baada ya kukabidhiwa na kutangazwa rasmi kuwa mabingwa wa michuano
hiyo kwa netiboli.
Wachezaji wa timu ya Bunge la Uganda wakifuahia kukabidhiwa Kombe lao baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika Soka.
Mwandishi
wa habari wa TBC Gerson Msigwa akimhoji Rais wa Uganda Yoeri Museven
ambaye alisema timu zote zilizocheza mashindano hayo ni watoto wake na
kwamba ushindi ni wa Afrika Mashariki.
Rais Yoeri Museveni akifurahia pamoja na wachezaji wa timu ya bunge la Tanzania baada ya kupata ubingwa katika netiboli.
Wachezaji wa timu ya Bunge la Uganda wakifuahia kukabidhiwa Kombe lao baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika Soka.
*******
Timu ya Netiboli ya Bunge la Tanzania imefanikiwa kuibuka mabingwa kwa mara ya pili mfurulizo katika michuano ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyofanyika Jijini Kampala nchini Uganda kuanzia Desemba 07,2013 mwaka huu.
Fainali za michuano hii zimefanyika katika uwanja wa Mandela Namboole jijini Kampala Uganda.
Bunge Tanzania imenyakua ubingwa huo baada ya kuichalaza timu ya wenyeji Bunge la Uganda kwa Jumla ya Mabao 35-32, na hivyo kutetea kombe lake ililoshinda kuanzia mwaka jana.
Mshindi wa tatu timu ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki imefanikiwa kuchukua nafasi ya tatu baada ya kuichapa timu ya Bunge la Kenya.
Katika Soka timu ya Bunge la Uganda imefanikiwa kutetea ubingwa wake kwa mara ya tatu mfurulizo baada ya kuichapa timu ya jumuiya ya Afrika Mashariki 3-0, mshindi wa tatu katika Soka ni timu ya Bunge la Kenya iliyoichapa timu ya Bunge la Rwanda 2-1
Rais wa Uganda Yoeri Kaguta Museven alikua mgeni rasmi katika fainali za mashindano haya ambapo amesema anafurahishwa na jinsi mashindano yanavyowaleta wana Afrika Mashariki pamoja na kwamba mshindi wa mashindano haya ni Afrika Mashariki. Museven pia amesema anawapongeza wote huku akisema nchi zote ni watoto wake.
Post a Comment