Chama Cha
Mapinduzi kimeipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini kwa kazi iliyofanya
kuufikisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya hapa ulipofika. Akizungumza
katika mahojiano maalumu na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya Tume
kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba Nape alisema;
“CCM
inaipongeza Tume kwa kazi waliofanya, tunatambua kazi kubwa waliyofanya,
wamekamilisha kazi waliyotumwa salama na kwa wakati. Sasa tuwaachie wanaondelea
na mchakato yaani bunge la katiba na hatimaye wananchi. Tunautakia kila lakheri
mchakato huu, utumike kutuunganisha watanzania badala ya kutugawa” amesema Nape
Kuhusu
pendekezo la Tume la muundo wa Muungano wa serikali tatu Nape anasema;
“Tumesikiliza
hoja za tume juu ya sababu za kuendelea kupendekeza muundo wa serikali tatu,
tumezisikia, tutazichukua,kuzipeleka kwenye vikao vya Chama baada ya tafakuri
ya kutosha tutaamua ipasavyo” alisisitiza Nape.
Aidha Nape
alitumia nafasi hiyo kuwatakia watanzania kila lakheri kwenye mwaka mpya wa
2014.
Post a Comment