"Kwa
nini tunakuwa wepesi kudanganyika kiasi hiki? Yaani leo AG amesema,
tena kirahisi kabisa kwamba ZZK hana majina ya mabilionea wetu walioweka
mapesa huko nje na watu ghafla ahaaaa, huyu jamaa kumbe ni mwongo?
Swali la kwanza kabla ya kumshabikia AG ni je kuna wenzetu wenye
mabilioni katika akaunti za nje? Kama hivyo hizo hela ziliendaje? Hakuna
watu wenye hizo akaunti? Na kama wapo nani mwenye jukumu la kuwajua-ni
serikali, mbunge au raia yeyote?
Ripoti iliyotolewa mwaka
jana na Benki Kuu ya Uswisi (Swiss National Bank) ilionyesha kwamba
watazania wana fedha zipatazo dola za kiamerikani 196 millioni, lakini
hawakutaja majina ya wenye akaunti hizo. Kwa hiyo kwamba kuna watanzania
walioficha mahela huko nje sio hisia, ni jambo la kweli. Swali ni nani
mwenye jukumu la kuwataja hao watu? Kwa nini serikali inakwepa wajibu?
Tuachane na siasa nyepesi nyepesi. Tuanze kuuliza maswali angalau
marahisi kwa kuanzia. Tunajaribu kujenga hoja kwamba kila chuo kikuu
hapa nchini kianze kufundisha somo la critical thinking kwa kila
mwanafunzi!"
Ripoti iliyotolewa mwaka jana na Benki Kuu ya Uswisi (Swiss National Bank) ilionyesha kwamba watazania wana fedha zipatazo dola za kiamerikani 196 millioni, lakini hawakutaja majina ya wenye akaunti hizo. Kwa hiyo kwamba kuna watanzania walioficha mahela huko nje sio hisia, ni jambo la kweli. Swali ni nani mwenye jukumu la kuwataja hao watu? Kwa nini serikali inakwepa wajibu?
Tuachane na siasa nyepesi nyepesi. Tuanze kuuliza maswali angalau marahisi kwa kuanzia. Tunajaribu kujenga hoja kwamba kila chuo kikuu hapa nchini kianze kufundisha somo la critical thinking kwa kila mwanafunzi!"
Post a Comment