Gadi
ya Wanaume ya Jeshi la Magereza ikipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama(hayupo pichani)katika mwendo wa haraka kama inavyoonekana katika
picha.
Gadi
ya Wanawake ya Jeshi la Magereza ikiwa katika mwendo wa pole kama
wanavyoonekana katika picha wakipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama(hayupo pichani).
Baadhi
ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza walioshiriki kikamilifu
Gwaride rasmi la Maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika
wakisakata rumba mara baada ya kumaliza shughuli ya Paredi. Hafla hiyo
fupi iliandaliwa na Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja kwa
lengo la kuwapongeza Makamanda hao kutokana na umahiri, ukakamavu
waliouonyesha katika Gwaride la Maadhimisho ambapo hafla hiyo imefanyika
katika Ukumbi w Bwalo Kuu la Maafisa wa Magereza, Ukonga Dar es Salaam.
Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Gideon Nkana akitoa hotuba fupi kwa
niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza kwa Washiriki wa Gwaride
rasmi la Maadhimisho ya Miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika(hawapo
pichani). Hafla hiyo fupi imefanyika jana Desemba 09, 2013 katika Ukumbi
wa Bwalo Kuu la Maafisa wa Magereza, Ukonga Dar es Salaam.
Baadhi
ya Wataalam wa Magwaride wa Jeshi la Magereza wakisikiliza hotuba ya
Mgeni rasmi wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza Washiriki wote wa
Gwaride la Maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika. Hafla hiyo
fupi iliyoandaliwa na Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja
kwa lengo la kuwapongeza Makamanda hao imefanyika jana Desemba 09, 2013
katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa wa Magereza, Ukonga Dar es
Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Post a Comment