|
Kamaba tayari kwa kuchomwa |
|
viongozi
wa Muungano wa jamii Tanzania[MUJATA]akiwemo Soja Masoko,Abdul
Aziz,Diwani Kata ya Mwakibete Lucas Mwampiki na Chifu Shadrack Merere
kutoka Mbarali. |
|
Kamaba tayari kwa kuchomwa |
|
mwenyekiti wa mtaa Bwana Ndongole Mwatebele akitoa maelezo mafupi kwa machifu |
|
Chifu
Merere alitaka amani katika mtaa huo na kuamua kuiteketeza kamba kwa
moto huku umati ukishuhudia tukio hilo na chifu kuahidi kumrejesha kwa
mazingara eneo la Mwakibete ili ajibu tuhuma zinazomkabili mtuhumiwa
huyo |
|
Wakazi wa Mwakibete wakishuhudia kuchomwa kwa kamba hiyo
Imani
za kishirikna zimezidi kuchukua sura mpya mkoani Mbeya baada ya
mwanamke aliyefahamika kwa jina la Lucy Frank[55]mkazi wa Manyoni
Singida kudai kamba iliyotumika kushushia jeneza la marehemu dada yake
apewe ili aende nayo Singida.
Kauli
hiyo aliitoa katika msiba wa marehemu dada yake aliyefahamika kwa jina
la Elizabeth Sibonike[81] aliyefariki ghafla Novemba 19 mwaka huu katika
mtaa wa Viwandani kata ya Mwakibete na mazishi yake kufanyika Novemba
21 mwaka huu.
Baada
ya mazishi Lucy alidai dada yake kuwa kadhalilishwa kwa kuzikwa kwenye
jeneza kubwa na kushushwa kaburini kwa kutumia kamba aina ya
manila,akidai vijana walimtuhumu marehemu kuwa ni mshirikina hali
iliyomkasirisha.
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke Lucy Frank alitamka msibani kuwa
yeyote aligusa kamba makaburini atakufa hali ambayo iliwaudhi wakazi wa
mtaa huo na kumtaka mwenyekiti wa mtaa Bwana Ndongole Mwatebele
kuichukua kamba hiyo na kuitisha mkutano wa hadhara ili mwanamke huyo
kutoka Manyoni aeleze umma sababu za kitaka kamba hiyo.
Hata hivyo wananchi wa mtaa wa Viwandani wakitafakari hayo kijana mmoja miongoni mwa waliokamata kamba makaburini aitwaye
Julius Mwandambo alifariki kwa kugongwa na gari eneo la mama John
Desemba 15 mwaka huu hali iliyowafanya wananchi kutaharuki.
Wakati
taratibu za mazishi zikiendelea Desemba 16 wakati picha ya marehemu
ikitembezwa barabarani mtoto wa Lucy alisikika akisema kama aliyefariki
ni huyu, bado wengine watafuata hali iliyowafanya vijana kugoma kuchimba
kaburi mpaka atafutwe huyo mama na mwanae ili waeleze kauli zao zina
mantiki gani.
Katika
hali hiyo ya mtafaruku mama huyo na mwanae walienda kuhojiwa kituo cha
Polisi kati ambapo mtoto alikiri kutamka maneno hayo ingawa alisema kuwa
hakujitambua hivyo anaomba radhi.
Huku
wananchi wakimsubiria mwanamke huyo na mwanae kwenye mkutano ilidaiwa
kutoroka kwenda Singida na kwamba wananchi hawako tayari kuwaona warudi
mtaani hapo.
Mkutano
ulioitishwa Desemba 27 mwaka huu ulioitishwa na viongozi mbalimbali
wakiwemo viongozi wa Muungano wa jamii Tanzania[MUJATA]akiwemo Soja
Masoko,Abdul Aziz,Diwani Kata ya Mwakibete Lucas Mwampiki na Chifu
Shadrack Merere kutoka Mbarali.
Chifu
Merere alitaka amani katika mtaa huo na kuamua kuiteketeza kamba kwa
moto huku umati ukishuhudia tukio hilo na chifu kuahidi kumrejesha kwa
mazingara eneo la Mwakibete ili ajibu tuhuma zinazomkabili
Na Ezekia Kamanga
Mbeya yetu
|
on Monday, December 30, 2013
Post a Comment