Mkazi
wa Mjimwema, Kasto Komba (45), amepandishwa kizimbani kujibu shitaka
la kutishia kuwaua mke na mama mkwe kwa kuwachongea jeneza na msalaba
wenye majina yao.
Waliotishiwa maisha yao ni Spensiana Mbawala (26) na mama mkwe Tisiana Mbawala (43), ambao waliwekewa jeneza hilo kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi.
Akisoma shitaka hilo mwanasheria wa serikali, Amina Mawoko, mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa, Elizabeth Misana, alisema kuwa Desema 14, mwaka huu majira ya saa 4 usiku huko katika eneo la mji mwema manispaa ya Songea, Kasto Komba, alitishia kuwaua mama mzazi wa mke wake.
Mawoko alifafanua kuwa mshitakiwa Komba alichonga jeneza pamoja na msalaba ambao aliandika majina ya walalamikaji na kulipeleka kwenye nyumba ambayo walikuwa wanaishi zamani.
Alidai kuwa baada ya kulipeleka jeneza hilo, mshitakiwa alitoroka na kutokomea kusiko julikana na kwamba baadae wapangaji wanaoishi kwenye nyumba hiyo walipoamka asubuhi walishtuka kuliona jeneza mlangoni na kutoa taarifa kwa wahusika ambao walifika eneo la tukio na kwenda kuripoti polisi.
Upande wa mashitaka umedai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Komba wakati anaishi na mke wake kipindi cha nyuma alikuwa hatoi huduma ndipo mkewe huyo aliamua kurudi kwao kitendo ambacho Komba hakukubaliana nacho na kumtaka arudi nyumbani ili waendelee kuishi pamoja, lakini mkewe huyo alikataa.
Alisema walalamikaji walipoona wanasumbuliwa waliamua kuhama kwenye nyumba hiyo ndipo mshitakiwa alipoamua kuchonga jeneza na msalaba na kulipeleka kwenye nyumba waliyohama walalamikaji hao.
Hata hivyo mshitakiwa alikana shitaka hilo na yupo nje kwa dhamana ya Sh. 300,000. Kesi imehairishwa hadi Desemba 19, mwaka huu itakapoletwa kwa hukumu.

CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment