Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MALKIA MAXIMA WA UHOLANZI AWASILI NCHINI .... JK AMFANYIA HAFLA YA NGUVU



Malkia  Maxima wa Uholanzi akiwa amefuatana na Mwenyeji wake Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. Mwingine pembeni ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Raymond Mushi.

Malkia Maxima kwa pamoja na Mhe. Mama Salma wakifurahia burudani kutoka kwa mojawapo ya vikundi vilivyokuwepo uwanjani wakati wa mapokezi. 
D92A2780
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akigonga glasi na Malkia wa Uholanzi Maxima wakati wa dhifa aliyoiandaa kwaajili ya Malkia huyo na ujumbe wake ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni(picha na Freddy Maro)


Wakuu wa Wilaya za Kinondoni na Temeke, Mhe. Jordan Rugimbana (wa nne kutoka kushoto) na Mhe. Sophia Mjema (wa tatu kutoka kushoto) wakiwa uwanjani hapo wakati wa mapokezi ya Malkia Maxima. Wengine ni Balozi Dora Msechu (kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Victoria Mwakasege (wa pili kutoka kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika na Bw. Songelaeli Shila, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa  katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mhe. Mama Salma akimtambulisha kwa Malkia Maxima  Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Ne na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu. Pembeni kwa Balozi Msechu ni Bibi Victoria Mwakasege, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Ulaya na Amerika

Malkia Maxima kwa pamoja na Mama Salma wakifurahia  wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshoghulikia masuala ya Chakula (WFP), Bi. Ertharin Cousin akiwaeleza jambo mara baada ya Malkia Maxima kuwasili nchini.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini, Dkt. Alberic Kacou (kushoto) akiwaeleza jambo Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Wilson Masilingi (katikati)  na Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe. Jaap Frederics wakati wa mapokezi ya Malkia Maxima wa Uholanzi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top