Malkia wa Uholanzi Mhe. Maxima
--
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
--
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Malkia wa Uholanzi Mhe. Maxima anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 11 Desemba, 2013 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Mhe.
Maxima ambaye pia ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa katika masuala ya Mfumo Jumuishi wa Fedha katika Maendeleo
atapokelewa na mwenyeji wake, Mke wa Rais, Mhe. Mama Salma Kikwete
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Baada
ya kuwasili, Mhe. Maxima atafanya mazungumzo rasmi na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu, Dar es
Salaam pamoja na kushiriki katika Dhifa ya Kitaifa.
Aidha,
tarehe 12 Desemba 2013, Malkia Maxima atafanya mazungumzo na Waziri wa
Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Mhandisi Christopher Chiza, Naibu
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada M. Salim na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania,
Prof. Benno Ndulu.
Siku
hiyo hiyo Mhe. Maxima atazindua rasmi Mfumo Jumuishi wa Fedha wa Taifa
katika hafla itakayofanyika Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Mfumo huo
unalenga kuwanufaisha Wanawake na Vijana, hususan katika kuchangia
usalama wa chakula, kilimo na maendeleo Vijijini.
Mhe.
Maxima ataondoka Dar es Salaam tarehe 13 Desemba, 2013 kuelekea Dodoma
ambako ataendelea na ziara yake kwa kutembelea mashamba ya zabibu katika
Kijiji cha Gawaye pamoja na kuzungumza na Wakulima. Mashamba hayo
yanasimamiwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Chakula Duniani (WFP),
Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) na Mfuko wa Kimataifa wa
Maendeleo ya Kilimo (IFAD).
Mhe. Maxima anatarajiwa kuondoka nchini siku hiyo hiyo jioni kurejea Uholanzi.
IMETOLEWA NA:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM.
10 DESEMBA, 2013
Post a Comment