Mbunge wa
jimbo la Isimani ambae ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na
uratibu wa bunge Bw Wiliam Lukuvi kulia akimkabidhi msaada wa gari la
wagonjwa mganga mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Ignesa Mlowe kwa ajili ya
kituo cha afya Kimande gari lenye thamani ya Tsh milioni 180
lililotolewa na serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii
Mbunge wa
jimbo la Isimani ambae ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na
uratibu wa bunge Bw Wiliam Lukuvi akimkabidhi msaada wa fedha kiasi cha
Tsh milioni 2.2 kwa ajili ya kusafisha mfereji wa umwagiliaji anayepokea
kulia ni mwenyekiti wa jumuiya ya wakulima wea mpunga katika mfereji wa
Mlenge Bw Fundi Maleva leo
Mbunge wa
jimbo la Isimani ambae ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na
uratibu wa bunge Bw Wiliam Lukuvi akijaribu pikipiki mbili zilizotolewa
na rais Dr Jakaya kikwete kwa jumuiya ya watumiaji maji Pawaga .
Na FRANCIS GODWIN BLOG,IRINGA
MBUNGE wa
jimbo la Isimani mkoani Iringa Wiliama Lukuvi amekabidhi gari la
wagonjwa lenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 180 kwa kituo cha afya
Kimande Pawaga na kumwondoa aliyekuwa dereva wa gari la awali ambaye
alituhumiwa kupakia meno ya tembo katika gari la wangonjwa.
Hata
hivyo alisema kuwa hakuna mwenye uhakika na tuhuma za dereva huyo
kujihusisha na kitendo cha kubeba meno ya tembo kupitia gari la wagonjwa
kama ambavyo moja kati ya magazeti hapa nchini yalipata kutoa tuhuma
hizo kwa dereva huyo.
"Nimeamua
kutumia busara zaidi kumwondoa dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo la
wagonjwa na kumweka mwingine kutokana na upotoshwaji uliofanywa na moja
kati ya magazeti kwa kuandika kuwa dereva huyo anabeba meno ya tembo
katika gari hilo ....japo tambueni kuwa sifa mbaya si kwa dereva ni kwa
wananchi wote wa tarafa ya pawaga ila tumemleta dereva mwingine"
Huku
akimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kutekeleza ahadi yake ya pikipiki na
ujenzi wa majengo ya jumuiya ya watumiaji maji pamoja na kutoka usafiri
wa pikipiki wa viongozi wa jumuiya hiyo.Akizungumza leo na wananchi wa
tarafa ya Pawaga baada ya kukabidhi msaada wa gari hilo la wagonjwa
ambalo limetolewa na wizara ya afya , Lukuvi alisema kuwa magari kama
hayo yametolewa katika maeneo mbali mbali ya nchi na katika mkoa wa
Iringa ni gari moja pekee ndilo limetolewa kwa wananchi wa Pawaga.
Hata
hivyo alisema kuwa anampongeza waziri wa afya na ustawi wa jamii Dr
Husein Mwinyi ambae alifika katika eneo hilo akiwa naibu waziri wa afya
na kuahidi kutatua kero ya vifo vya wanawake wajawazito ambavyo vilikuwa
vikitokea kutokana na eneo hilo kukosa gari la wagonjwa .
Kuhusu
huduma ya maji katika eneo la Mlenge alisema kuwa kiasi cha Tsh bilioni 2
zinahitajika kwa ajili ya wananchi wa eneo hilo la Mlenge ambao kwa
sasa hawanahuduma ya maji.
Alisema
jumuiya ya watumiaji maji ya Pawaga inayonafasi ya kutumia vema mradi
huo wa maji ili ikiwezekano kuwezesha wananchi wa jirani na kijiji hicho
kuweza kupata huduma ya maji na kuwa wasisite kuwachukulia hatua
wafugaji jamii ya kimasai na wasukuma ambao wameendelea kuhujumu miundo
mbinu ya maji kwa kukata mabomba ya maji.
Lukuvi
ambae ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge
alisema kuwa ndoto yake ya maendeleo katika jimbo hilo hasa pawaga ni
kuona wananchi wa eneo hilo wanaunganishwa na barabara ya uhakika na
badala ya kwenda mjini Iringa kupata usafiri sasa wakatengenezewa
barabara itakayounganisha eneo hilo na barabara ya Iringa- Dodoma.
Alisema
kuwa zipo fedha ambazo zimetolewa na ofisi ya waziri mkuu kwa ajili ya
kuwa na barabara za mfano kwa ajili ya kuinua uchumi wa wananchi wa
Halmashauri ya wilaya ya Iringa ambapo katika mradi huo watahakikisha
wanajenga ghara la kuhifadhia mazao ya wakulima hasa zao la mpunga.
Lukuvi
alisema kuwa timu ya wataalam itafika katika eneo la Pawaga ili kutoa
elimu kwa wakulima wa mpunga ili kuboresha zaidi kilimo na soko la
mchele wao kupitia mradi huo ambao umetengewa fedha na ofisi ya waziri
mkuu.
Wakati
huo huo Lukuvi amekabidhi msaada wa Tsh milioni 2.2 kwa wakulima
wanaotumia mfereji wa umwagiliaji wa Mlenge ili mtambo wa kusafisha
mfereji huo baada ya kuombwa na wananchi hao wa tarafa ya pawaga
on Monday, December 16, 2013
Post a Comment