Muwakilishi
wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,
Balozi Tuvako Manongi ameungana na Wawakilishi wa Mataifa
mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa, katika
kusaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa Kwanza wa
Afrika ya Kusini Huru, Mzee Nelson Mandela.
Kitabu
hicho kimefunguliwa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Afrika
ya Kusini katika Umoja wa Mataifa. Katika Salamu zake, Balozi Tuvako
Manongi ameandika " kwa niaba ya Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, ninawasilisha salamu zetu
za rambirambi kwa serikali, wananchi, familia na wapendwa wa Marehemu
Mhe. Mzee Nelson Mandela.
Tunaungana
nanyi katika kuombeleza msiba wa kiongozi huyo ambaye alijitolea
katika kuikomboa Afrika ya Kusini. Mchango wake katika kuwaunganisha
wana wa afrika ya kusini licha ya tofauti zao za kikabila ni jambo
lililoihamasisha dunia yote. Sisi katika Tanzania tunajivunia sana
kumfahamu Madiba".
Post a Comment