Dar
es Salaam. Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewataka watanzania kuacha tabia
ya kuwa na roho ya kulipiza visasi badala yake wawe watu wa kusamehe na
kusahau kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanamuenzi moja kwa moja Rais
mstaafu wa Afrika Kusini Marehemu Nelson Mandela.
Rais
Kikwete amesema mara baada ya Rais Mandela kutolewa gerezani hofu
ilitawala Afrika ya Kusini, watu wengi wakitambua kuwa atakapochaguliwa
kuwa Rais badala ya kuijenga nchi ataanza kulipiza visasi kwa wale wote
waliotumika kwa namna moja ama nyingine kumtesa yeye na watu wa nchi
yake.
“Badala
yake Mzee Mandela alitoa tamko la kuwasamehe wote waliohusika kuwabagua
watu wa Afrika ya Kusini, na kisha aliunda tume maalumu ya maridhiano
ili kujenga umoja kati ya watu wenye ngozi nyeupe na wenye ngozi nyeusi,
jambo hili ni la ajabu sana” amesema Kikwete.
“Hiki
ni kipimo kikubwa cha ukomavu wa kisiasa, yatupasa watanzania na
viongozi mbalimbali kuenzi jambo hili la kusameheana na kutokuwa
walipiza visasi, hapa tulipo wengine wanasema kabisa nikichaguliwa
watanikoma….. lakini nawasihi tumuenzi Mzee Mandela kwa kuiga mambo mema
aliyoyafanya ambayo hadi hivi leo yamechangia kukuza uchumi wa Afrika
ya Kusini, “amesema Kikwete.
Amesema
tokea enzi za TANU Tanzania imekuwa karibu sana na vyama vya ukombozi
wa mataifa mengi Afrika, kikiwemo chama cha ANC ambacho kilikuwa
kikiongozwa na Marehemu Mzee Mandela, hivyo aliwasihi watanzania
waendeleze umoja huo .
“Kuna
jambo moja ambalo hamlijui mwaka wa 1964 Mzee Mandela alikuja nchini na
kufikia kwa mweka hazina wa TANU, Siro Swai, alikuwa akielekea kwenye
mafunzo ya kijeshi Algeria, aliacha viatu vyake ‘pea moja’ akieleza kuwa
atakaporudi atakuja kuvichukua lakini haikuwa hivyo, nilipokuwa waziri
wa mambo ya nje, mke wa Swai alinifuata na kunieleza, nasi tulilazimika
kuzirudisha kipindi hicho ambacho Mzee Mandela alikuwa Rais wa nchi hiyo
tayari,” Anaeleza Kikwete.
Amesema
haya yote yanatafsiri ukaribu na undugu wa hali ya juu kati ya nchi
zetu mbili na ndiyo maana katika kumuenzi leo hii kwenye shughuli za
kutimiza miaka 52 ya uhuru hatutakuwa na vikundi vya kutumbuiza.
Kwa habari Zaidi ungana nasi baadaye.
Ibada maalumu ya Mandela
Johannesburg.
Afrika Kusini, jana ilitawaliwa na ibada na maombi yaliyofanyika katika
makanisa mbalimbali kuliombea taifa, baada ya kifo cha Rais wa Kwanza
mzalendo, Nelson Mandela
on Monday, December 9, 2013
Post a Comment