Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw.Eliakim Maswi, akizungumza
na Mhariri wa mtandao wa habari wa MOblog Damas Makangale katika
mahojiano maalum kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar. Kushoto ni
Mwandishi kutoka Idara ya Habari Maelezo Frank Shija.
Katibu Mkuu wa Kwanza kutamba kwamba rushwa kwake mwiko
.awataka watanzania kujitokeza katika uchimbaji na utafutaji gesi asilia
.asema waache kulalamika
.aahidi kuendelea kusimamia maslahi ya Taifa
.Wizara yake yaanda mkakati wa kuwakopesha wachimbaji wadogo wa madini nchini
Na Damas Makangale, MOblog
KATIBU
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw,.Eliakim Maswi mwishoni mwa
juma alivunja ukimya na kutamka bayana kwamba wazawa wanaruhusiwa
kuingia katika biashara ya kimataifa ya utafutaji na uchimbaji wa Gesi
asilia nchini.
Akizungumza
na MOblog katika mahojiano maalum baada ya kufunguka mkutano wa mwaka
wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini na Nishati (Tanzania Chamber of
Minerals and Energy) amesema kuna upotoshaji ukubwa kwamba serikali
inazuia wazawa kufanya biashara ya utafutaji na uchimbaji wa Gesi
asilia.
“Serikali
ipo tayari kuzungumza na kuwapa vitalu baada ya kulipia wazawa wote
wenye nia ya kuingia katika biashara hii ya kimataifa ya uchimbaji wa
Gesi asilia hatuna matatizo na wazawa ambao wana nia ya kuingia katika
biashara hii,” amesema
Maswi
alilisitiza kwamba Mtanzania anapaswa kulipa Dola za kimarekani 700,000
ili apatie kitalu na ni bei ya chini tofauti na mwekezaji kutoka nje.
Alisisitiza
kwamba Wizara ya Nishati na Madini ipo tayari kufanya kazi na wazawa
katika sekta ya gesi asilia kwa sababu ufumbuzi wa madini hayo
yataharakisha maendeleo ya Taifa katika Nyanja zote za uchumi.
Tukiharakisha
uchimbaji wa gesi asilia itaongeza kasi ya kuondoa umasikini wa
wananchi hasa katika maeneo ambayo gesi inapatikana,” aliongeza Maswi
Maswi
amesema ingawa uchimbaji na utafutaji wa gesi asilia na utafiti
(Exploration) kuhitaji mtaji mkubwa na wa muda mrefu ndiyo maana wizara
ikaamua kupunguza gharama ya kitalu kwa wazawa ili kuwapa fursa murua ya
kuingia katika biashara hiyo.
Kwa
upande wa madini, Maswi amesema Wizara ya Nishati na Madini inaandaa
mpango mkakati kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo nchini (TIB) ili
waweza kukopeshwa na kuongeza mitaji katika biashara zao za madini
nchini.
“tupo
katika hatua za mwisho na uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Taifa (TIB)
ili waweze kuwakopesha wachimbaji wadogo wadogo wa madini nchini kwetu,
wizara inawajali wazawa jamani alisisitiza,”
Wakati
huo huo, hivi karibuni Rais wa Jakaya Kikwete alinukuliwa akisema
kwamba maandalizi ya uchimbaji gesi nchini Tanzania yasichukue muda
mrefu kwa sababu wananchi wanahitaji kuona manufaa ya Gesi asilia katika
kipindi kifupi iwezekanavyo na kwamba, makadirio ya miaka kumi ni mingi
sana.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameongeza kuwa, gesi asilia
inayoendelea kugunduliwa nchini humo ni rasilimali muhimu na ni lazima
itumike katika kuwatoa Watanzania katika umasikini na kwamba, ni lazima
rasilimali hiyo ibadilishe maisha ya wananchi.
Post a Comment