Nchi ya Tanzania imeingia tena kwenye
headline kuhusiana na suala la Madawa ya kulevya baada ya kukamatwa tena
kwa Mtanzania mwingine akisafirisha Madawa hayo toka Thailand kuelekea
Macao nchini China jumanne iliyopita.
Mtanzania huyo ni msichana ana jumla
ya umri wa miaka 28 aitwae Jackie Clief alikamatwa na kilo 1.1 za dawa
za kulevya aina ya Heroin huko Macao nchini China
Dawa hizo zimekutwa tumboni mwake
baada ya kushtukiwa na wana usalama kisha kufanyiwa X-ray ambapo baada
ya kufanyiwa X-ray alikutwa na jumla ya vidonge 66 vikiwa na thamani ya
dola za kimarekani 137,72.
Msichana
huyu aliliambia Jeshi la Polisi nchini China kwamba alikua akisafiri
kuelekea Guangzhou ambao ni mji ulio chini ya jimbo la Guangdong huko
China,Inasemekana Msichana huyu amewahi kushiriki video mbalimbali ikiwa
ni pamoja na video ya Nataka kulewa ya Diamond.
Hii ni picha imepigwa akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Macao.
Jack Cliff mwenyewe ndio huyu hapa
1 comments:
There's no short cut in life tujifunze kutokana na mambo haya jamani tutafute ujuzi tuweze kujiri tatizo la drugs lazima litakurudia tuu km sio ww basi ata mtu wako wakaribu
ReplyPost a Comment