Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS DKT. KIKWETE AFANYA UTEUZI WA WAJUMBE WA BARAZA LA CHUO CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA

 


jk_taifa
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

TAARIFA KWA UMMA 
UTEUZI WA WAJUMBE WA BARAZA LA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA
        Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Prof. Penina Mlama kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya. Uteuzi huo ni kwa mujibu wa Sheria ya Vyuo Vikuu ya mwaka 2005 na hati idhini ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya. Uteuzi huo ni wa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10 Desemba, 2013.
        Aidha, kufuatia uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza hilo, Prof. Makame M. Mbarawa (Mb), Waziri mwenye dhamana ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, ambaye kwa mujibu wa hati idhini ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya na mamlaka aliyonayo amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Baraza la Chuo:
  1. Mhe. Dkt. Pindi Chana, Mbunge wa Viti Maalum-Njombe na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Sheria, Mwakilishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
  1. Eng. Peter Chisawilo, Rais wa Chemba ya Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo, Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Mwakilishi wa Sekta Binafsi;
  1. Dkt. Haji Mwevura Haji, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma, Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar, Mwakilishi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
  1. Bw. Bernard T. D. Mbonde, Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Mwakilishi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya;
  1. Prof. Evelyne Mbede, Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia;
  1. Bw. Mapunda Erick Chrisantus, Mhadhiri na Rais wa Chama cha Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Mwakilishi wa Chama cha Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya; na
  1. Bw. Augustine K. Olal, Kamishna Msaidizi wa Sera za Uchumi Mpana, Mwakilishi wa Wizara ya Fedha.
Uteuzi wa wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ni wa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10 Desemba, 2013.
Imetolewa na; 
Prof. Patrick J. Makungu, 
Katibu Mkuu, 
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top