Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni wakati aliposimama
kwa muda katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini
Nairobi akiwa njiani kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano
unaohusu Amani na usalama na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Bara la
Africa na Ufaransa.Kulia aliyesimama ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya
Balozi Amina Mohamed na kushoto ni afisa itifaki.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya
Balozi Amina Mohamed wakati aliposimama kwa muda katika uwanja wa ndege
jijini Nairobi, Kenya alipokuwa akirejea nyumbani akitokea Paris
Ufaransa ambapo alihudhuria Mkutano uliohusu Amani,Usalama na
Ushirikiano wa kiuchumi kati ya Ufaransa na bara la Afrika.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Mec Sadik akimkaribisha Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere muda mfupi baada y kuwasili akitokea Paris Ufaransa
ambapo alihudhuria Mkutano wa Amani,Usalama na Ushirikianokati ya Afrika
na Ufaransa uliomalizika jana.(picha na Freddy Maro)
Post a Comment