Rais wa Marekani Barack Obama leo Jumanne ameungana na Waafrika Kusini
katika kumkumbuka rais wa zamani wa taifa hilo Nelson Mandela ambapo
amemsifia na kumtaja kama mkongwe wa historia ambaye amepata nafasi hiyo
katika vizazi kupitia mapambano, msimamo imara katika maamuzi, na kwa
kuonyesha uwezo katika maamuzi ya kisiasa.
Obama amemtaja Mandela kama kielelezo cha jinsi gani watu wanaweza
kufikia mabadiliko kwa kupigana kwa ajili ya maadili yao na kujenga hoja
na sababu kufikia kujitoa kwao.
Obama amesema kuwa ni vigumu kumsifia mtu yeyote , lakini ni vigumu
zaidi kufanya hivyo hasa kwa mkongwe wa historia , ambaye amelifikisha
taifa katika haki,na mtu aliyemfanya yeye ashawishike kuingia katika
siasa, Nelson Mandela.
Aidha rais Obama amesema kuwa kifo cha Mandela kikumbukwe kwa kipindi
cha maombolezo lakini pia kikumbukwe kwa kipindi cha kuhamasisha wakati
watu wakitazama jinsi gani wanaweza kubadilisha maisha yao.
Rais Obama amefuatana na marais watatu wa zamani wa Marekani Jimmy
Carter, George W. Bush na Bill Clinton,katika shughuli hiyo maalum.
Post a Comment