|
Mpiga picha wa Clouds TV akiwajibika kuchukua tukio la ubovu wa stendi ya Njombe |
|
Abiria wakipita kwa shida katika stendi ya Njombe |
|
Madereva
na abiria wanaotumia stendi ya Njombe mjini ambayo ni stendi kuu
ya mabasi yaendayo mikoani wamelalamikia ubovu wa stendi hiyo na
kumwomba mbunge wa jimbo hilo Anne Simamba Makinda kushughulikia
tatizo hilo.
Wakizungumza na mtandao huu wa
www.francisgodwin.blogspot.com madereva hao na wananchi walisema
kuwa ubovu wa stendi hiyo umekuwa ni kero kubwa kwao na kuiomba
Halmashauri ya mji wa Njombe kulishughulikia suala hilo
John
Sanga ni mmoja kati ya madereva eneo hilo la stendi alisema kuwa
wameshangazwa na hatua ya mbunge wao ambae ni spika wa Bunge
kushindwa kuwajibika kwa kusimamia utengenezaji wa stendi hiyo.
Kwa
alisema wakati wa jua eneo hilo limekuwa likiongoza kwa kuwa na
vumbi na wakati wa masika linaongoza kwa kuwa na tope sana .
Hata
hivyo alisema kuwa uongozi wa serikali ya Njombe umekuwa ukitoa
ahadi ya kutengeneza stendi bila kutekeleza kwa wakati na pale
madereva wanapotaka kugoma wamekuwa wakitumia polisi kuwakamata
waanzilishi wa migomo hiyo.
Huku Sarah Ndelwa ambae ni mmoja
kati ya abiria waliohojiwa akimtaka mbunge Makinda kusaidia kuondoa
aibu hiyo ya ubovu wa stendi nyumbani kwake |
on Saturday, December 28, 2013
Post a Comment