TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa itashiriki katika hafla ya makabidhiano ya magari ya msaada
kutoka Serikali ya China katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, tarehe 31 Desemba 2013, saa 3:00 asubuhi.
Hafla hiyo itahudhuriwa na Uongozi wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Wizara ya Fedha,
pamoja na Ubalozi wa China hapa nchini.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
30 Desemba, 2013.
Post a Comment