“PRESS RELEASE” TAREHE 12.12. 2013.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – AJALI YA GARI KUGONGANA NA PIKIPIKI NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 11.12.2013 MAJIRA YA SAA 17:05HRS HUKO MAENEO YA MBALIZI
BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA KATA YA BONDE LA SONGWE, TARAFA YA USONGWE,
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA. GARI T. 106 ARE AINA YA
TOYOTA HAICE LIKIENDESHWA NA DEREVA THOMAS S/O TIBEGIRE, MIAKA 43,
MHAYA, ASKARI WA JWTZ KIKOSI CHA 44 KJ MKAZI WA MBALIZI LILIGONGANA NA
PIKIPIKI STK 4245 AINA YA HONDA IDARA YA KILIMO UYOLE IKIENDESHWA NA
JUMA S/O MWASHALA, MIAKA 45, MMALILA, FUNDI MAGARI, MKAZI WA MBALIZI NA
KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI AKIPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI TEULE
YA IFISI. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA NAIBU KAMISHNA WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI NA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MNAMO
TAREHE 11.12.2013 MAJIRA YA SAA 18:00HRS HUKO STENDI KUU, KATA YA
SISIMBA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA WALIMKAMATA THADELA S/O HARGATHA, MIAKA 30, RAIA NA MKAZI WA
NCHINI ETHIOPIA AKIWA AMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MTUHUMIWA ALIKAMATWA
AKIWA ANAKULA CHAKULA KWENYE KIBANDA CHA MAMA LISHE. TARATIBU ZINAFANYWA
ILI AKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA NAIBU KAMISHNA WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA
WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU
WANAOWATILIA MASHAKA ILI TARATIBU ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE
[DIWANI ATHUMANI – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment