Mhe.
Balozi Tuvako Manongi akizungumza wakati wa mkutano wa pembezoni
uliokuwa umeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na
masuala ya Elimu, Sayansi na Utamaduni ( UNESCO) na Baraza la Kimataifa
la Sayani ICSU), Balozi Manongi alikuwa kati ya wanajopo wanne
walioongoza majadiliano hayo.Wengine kutoka kushoto ni Bi. Vibeke Jense
ambaye ni Mkurugenzi wa UNESCO Ofisi ya New York, katikati ni mwedesha
majadiliano na kulia kwa Balozi Manongi ni Bw. Gisbert Glaser Mshauri
Mwandamizi kutoka Baraza la Kimataifa la Sayansi ( ICSU).
Bw. Hassan Mshinda, ambaye ni Kamishna kutoka Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia akichangia katika majadiliano hayo.
sehemu ya washiriki wa mkutano huo.
Washiriki
wengine wakifuatili kwa makini majadilianyo hayo kuhusu nafasi ya
sayansi na teknolojia katika utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo
Endelevu, majadiliano hayo yaliandaliwa kwa ushirikiano wa UNESCO na
ICSU.
Muwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi
akibadilishana mawazo na Bw. Gisbert Gladser ambaye katika majadiliano
hayo, alitaka kufahamu Tanzania inatumiaje uzoefu wake na mafanikio
yaliyoainishwa katika majadiliano hayo kuzisaidia nchi nyingine za
Afrika akilenga katika uhusiano na ushirikiano baina ya nchi za Kusini (
South- South Cooperation ).
Na Mwandishi Maalum
Balozi
Tuvako Manongi, Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa
Mataifa, amesema, kwa kuwa sayansi na teknolojia ni suala mtambuka
basi tafiti na uvumbuzi unaofanywa na wanasayansi na wataalamu
mbalimbali hauna budi kujielekeza katika kujibu hoja na kuzitafutia
ufumbuzi changamoto zinazowakabili watu hususani katika kuondokana
na umaskini na kujiletea maendeleo endelevu.
Ametoka
kauli hiyo siku ya jumatatu wiki hii, wakati aliposhiriki katika
majadiliano ya pembezoni ( side event) yaliyokuwa yakijadili kuhusu
‘Sayansi kama tegemeo la baadaye la malengo ya maendeleo endelevu:
changamoto na fursa zake zake’.
Balozi
Maongi alikuwa kati ya wanajapo wanne katika majadiliano hayo
yaliyoandaliwa kwa pamoja baina ya Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni ( UNESCO) na Baraza la Sayansi la
Kimataifa ICSU). Wanajopo wengine walikuwa Mkurugenzi wa UNESCO
katika Umoja wa Mataifa, Bi Vibek Jensen, Bw. Gisbert Glaser ambaye ni
Mshauri Mwandamizi kutoka ICSU, na Bi. Paula Caballero,
Mkurugenzi wa masuala ya Uchumi, Jamii na Mazingira katika Wizara ya
Mambo ya Nje nchini Colombia.
“
Ninapozungumza na wazee wangu kule kijijini kwangu nilikozaliwa kuhusu
athari za uharibifu wa mazingira kwa kukata ovyo miti, swali
wanaloniuliza je unatupa mbadala gani . Hii ni sehemu ya changamoto
ambazo sayansi kupitia kwa wataalamu wetu wanatakiwa kutoa majibu au
kutoa njia mbadala za kuwafanya watu wanaotegemea miti kwa shughuli zao
wasiendele kufanya hivyo” akasema Balozi Maongi.
Na
kuongeza kwamba Tanzania kama iliyo kwa nchi nyingine zinazoendelea
inaamini kwamba sayansi na teknolojia inayonafasi na mchango mkubwa
sana katika kusimamia utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu
kutokana na ukweli kwamba suala hilo linagusa kila nyanja ya maendeleo
ya binadamu.
Hata
hivyo akabainisha kwamba licha ya mataifa mengi yakiwamo yaliyoendelea
kukiri umuhimu wa sayansi na teknolojia katika maendeleo, suala hilo
halikupewa umuhimu wakati wa utekelezaji wa Malengo ya Maendele ya
Millenia ( MDGs) yanayofika ukingoni mwaka 2015.
Na kwa
sababu hiyo akasema kwamba Tanzania ambayo ni miongoni mwa nchi 30
ambazo zimeteuliwa kushiriki katika majadiliano ya kiserikali ya
kuandaa malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015 (SDGs)
inatajitahidi kuchagiza suala la sayansi na teknolojia liingizwe katika
malengo hayo mapya hasa kipengere cha utekelezaji.
Mkutano
huo wa pembezoni umefanyika wakati ambapo wajumbe kutoka mataifa
mbalimbali duniani wapo hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ( New
York) kuhudhuria awamu ya sita ya majadiliano ya kiserikali ,
(Intergovenmental negotiations ) kuhuhusu Maandalizi ya Malengo Mapya
ya Mendeleo Endelevu ( SDGs) baada ya 2015.
Katika
majadiliano hayo Balozi Manongi alielezea uzoefu wa Tanzania katika
siyo tu utungaji wa serĂ¡ zinazosimamia masuala ya sayansi ya
teknolojia bali hata namna serikali kwa kushirikiana na wadau wa ndani
na nje iliyoweza kupanua wigo wa matumizi ya sayansi na teknolojia,
uongezaji wa ufadhili katika masomo ya juu katika eneo hilo pamoja na
uwezeshaji wa wanawake.
Akataja
pia changamoto mbalimbali ambazo Tanzania kama ilivyo kwa nchi
nyingine za Afrika inakabiliana nazo, baadhi ya changamoto hizo ni
pengo la teknolojia katika ya mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea,
tatizo la ubadilishanaji wa maarifa na wimbi la wataalam wa Afrika
kukimbili nje kutafuta maisha bora.
Na kwa
sababu hiyo akasema, pamoja na jitihada mbalimbali ambazo Tanzania
imezifanya na inaendelea kuzifanya katika eneo hilo la sayansi ya
teknolojia bado itaendelea kuhitaji misaada na ushirikiano wa karibu
hasa katika eneo la uwezeshaji na ubadilishanaji wa maarifa.
Katika
awamu hii ya sita ya majadiliano washiriki wanajikita pamoja na
masuala mengine kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu za utekelezaji
katika eneo la sayansi, teknolojia, ubadilishaji wa maarifa na
uwezeshaji na uhusiano wake na malengo mapya ya maendeleo endelevu.
Ujumbe
wa Tanzania katika majadiliano unaongozwa na Balozi Tuvako Manongi
ukiwahusisha Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Celestin Mush na Bw. Hassan Mshinda ambaye ni Kamishna kutoka
Kamisheni ya Sayansi na Teknlojia ( COSTECH).
Post a Comment