Kaimu Mhandisi wa Maji Manispaa ya
Temeke, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Meckiline
Haule (katikati) akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa
kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL) kwa gharama ya sh. mil. 35 katika Zahanati ya Kibada, Kigamboni,
Dar es Salaam juzi. Wanaoshuhudia ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo,
Isabela Ipopo (kushoto),Mwakilishi wa Mauzo wa TBL, Allen Mwebuga (wa
pili kushoto) na Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke,
Rumelius Bakilane
Kaimu Mhandisi wa Maji Manispaa ya
Temeke, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Meckiline
Haule (katikati) akipokea ufunguo kutoka kwa Mwakilishi wa Mauzo wa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Temeke, Allen Mwebuga (wa pili
kushoto) tayari kuzindua rasmi kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada
wa TBL kwa gharama ya sh. mil. 35 katika Zahanati ya Kibada, Kigamboni,
Dar es Salaam juzi. Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Zahanati
hiyo, Nassoro Sande (kulia) na Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Isabela
Ipopo.
Mwebuga wa TBL (kushoto) na Bakilane wakifujaza maji kwenye ndoo wakati wa uzinduzi wa kisima hicho.
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya
Temeke, Rumelius Bakilane akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Kijiji cha
Kibada, Diana Salvatory baada ya kampuni hiyo kukabidhi kisima cha maji
katika Zahanati ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kisima hicho
chenye uwezo wa kuhifadhi maji lita za ujazo 1,600 kwa saa uchimbaji
umegharimu sh. mil 35 zilizotolewa msaada na TBL.(P.T)
Mwakilishi wa Mauzo wa Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), Kanda ya Temeke, Allen Mwebuga akimtwisha ndoo ya maji
Mkazi wa Kijiji cha Kibada, Hidaya Mshindo baada ya kampuni hiyo
kukabidhi kisima cha maji cha msaada katika Zahanati ya Kibada,
Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kisima hicho chenye uwezo wa kuhifadhi
maji lita za ujazo 1600 kwa saa uchimbaji umegharimu sh. mil 35
zilizotolewa msaada na TBL.
Wakifurahi baada ya kuzindua kisima hicho
Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Ipopo
akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwasidia kisima hicho, hivyo kupunguza kwa
asilimia kubwa tatizo la maji katika zahanati hiyo.
Mkazi wa Kijiji cha Kibada akitoa shukrani wa TBL kwa msaada huo.
Wakazi wa Kibada wakiangalia kisima hicho
Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu
akielezea mikakati ya TBL kusaidia miradi ya maji nchini ambapo kwa
mwaka wafedha wa TBL tayari imetenga sh. mil. 450 kwa kazi hiyo.PICHA NA
KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Post a Comment