Mgeni
Rasmi katika sherehe za mwaka za Chama cha Wafanyabiashara wa Madini
Tanzania (Tanzania Chamber of Minerals and Energy) Katibu Mkuu Wizara ya
Nishati na Madini Eliakim Maswi akizugumza kwa niaba ya Waziri kwa
wageni waalikwa na mabalozi.(Picha na Zainul Mzige)
.Joseph Kahama aahidi ushirikiano na wachimbaji wadogo nchini
.Asema sekta ya madini kuongeza mchango wake kwenye pato la Taifa
Na Damas Makangale, MOblog
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini nchini (Tanzania Chamber of
Minerals and Energy) Joseph Kahama amesema chama kwa kushirikiana na
chuo cha Ufundi Veta Moshi wataendelea kupeleka vijana wazawa wa
kitanzania kwenda kupata mafunzo ya mambo ya uchimbaji na utafutaji wa
Madini (Geology).
Akizungumza
na MOblog jana kwenye mahojiano maalum baada ya kumaliza mkutano wao wa
mwaka kwa wanachama wake, Joseph Kahama amesema chama chao kwa
kushirikiana na serikali wataendelea kusaidia vijana wa kitanzania
kupata elimu ya kutosha katika sekta ya madini nchini.
“tumeshapeleka
vijana kadhaa kwenye mafunzo mahsusi ya madini na wengi wao wameshapata
kazi katika kampuni kadhaa za madini hapa Tanzania,” amesema.
Bw. Maswi akitoa neno na ahadi za serikali kuendelea kushirikiana wadau katika sekta ya madini nchini.
Mwenyekiti
wa Tanzania Chamber of Minerals and Energy, Joseph Kahama akizungumza
wakati wa sherehe hizo jana usiki katika hoteli ya Golden Tulip jijini
Dar es Salaam.
Kahama
alisisitiza kwamba si kweli kwa wageni wengi ndio wameajiriwa katika
sekta madini kuliko wazawa kwa sababu kwa takwimu asilimia 90
walioajiriwa sasa katika migoi mbalimbali ni watanzania.
Alisisitiza
kwamba wataendelea na mkakati wao wa kuwajengea uwezo wa sawa
(skills)katika uchimbaji na utafutaji wa madini ili kuongeza ajira kwa
vijana na kutokomeza umaskini hapa nchini.
Amesema
kwa sasa wana malengo kwa kushirikiana na serikali kuangalia kwa jinsi
gani wanasema kuongeza mchango wa sekta ya madini katika pato la taifa
kutoka 3.7 asilimia mpaka asilimia 10. Kahama
amesema kwamba kwa kushirikiana na serikali wataendelea kusukuma
gurudumu la maendeleo kupitia sekta ya madini na kuhakikisha kwamba
wazawa wananufaika vya kutosha kutokana na mchango wa sekta hiyo kwenye
uchumi wa taifa.
Amesema
pia wadau katika sekta hiyo wanawakaribisha wachimbaji wadogo wadogo
wawe wanachama wa chama chao ili waweze kusaidiana na kukabiliana na
changmoto mbalimbali. Kahama
aliahidi kwamba wanachama na wachimbaji wote wa madini watashirikiana
katika kuweka mazingira safi wakati wote wa utafutaji na uchimbaji wa
madini katika maeneo husika.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo Mabalozi wakifuatilia tukio hilo.
Wadau wa sekta ya madini nchini wakibadilishana mawazo kwenye Gala Dinner party ya wadau wa Sekta ya madini na Serikali iliyofanyika kwenye Golden Tulip jijini Dar.
Mgeni
Rasmi katika sherehe za mwaka za Chama cha Wafanyabiashara wa Madini
Tanzania (Tanzania Chamber of Minerals and Energy) Katibu Mkuu Wizara ya
Nishati na Madini, Eliakim Maswi akiongozana na Mwenyekiti
wa Tanzania Chamber of Minerals and Energy, Joseph Kahama kwenye meza
ya chakula wakati wa halfa ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Chama
cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Mwenyekiti wa Tanzania
Chamber of Minerals and Energy wakiongoza wageni waalikwa kupakua
chakula.
Wageni waalikwa wakijisevia chakula cha usiku.
Mwenyekiti wa Tanzania Chamber of Minerals and Energy, Joseph Kahama akibadilishana mawazo na wageni waalikwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akisalimiana na Mkurugenzi
Mtendaji wa Makampuni ya Ryan Bert and Compay Limited na Swordfish
Security Consultants Haki Ngowi liyeambatana na mdogo wake Mbunifu wa
mavazi nchini Sheria Ngowi.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akifurahi jambo na baadhi ya wageni waalikwa.
Mwenyekiti
wa Tanzania Chamber of Minerals and Energy, Joseph Kahama
akibadilishana mawazo na baadhi ya wadau wa sekta ya madini. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi na Wa pili kushoto Katibu Mkuu wa Tanzania Chamber of Minerals and Energy, Bw Emmanuel Jengo.
Makamu wa rais wa Africa Barrick Gold Bw. Deo Mwanyika (wa pili
kushoto) akibadilishana mawazo na Waheshimiwa mabalozi kwenye Gala
Dinner Party iliyoandaliwa na Tanzania Chamber of Minerals and Energy
kwenye hoteli ya Golden Tulip.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Eliakim Maswi akiteta jambo na Mmoja wa wadau katika sekta ya Madini.
Post a Comment