Abiria waendao mikoa mbalimbali wakiwa katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo.
*******
Hali ya usafiri katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo, imerejea kuwa ya kawaida.
Kwa takribani wiki moja ,kituo hicho kilikuwa katika hali mbaya ya usafiri, kutokana na kupungua kwa mabasi ya kwenda mikoani.
Mwananchi jana ilikwenda kituoni hapo na kushuhudia idadi ndogo ya abiria huku mabasi yakiwa mengi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Ofisa
kutoka Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (Chakua), Gervas Rutabuzinda,
alisema hali ya usafiri imerejea kama zamani.
“Tunashukuru Mungu hali ya usafiri imerejea kuwa ya kawaida,” alisema Rutabuzinda
Rutabuzinda alisema baada ya kumalizika kwa sikuku
za mwisho wa mwaka tatizo tatizo la usafiri litahamia mikoani, kwani
abiria wengi watakuwa wanarejea Dar es Salaam.
MWANANCHI
Post a Comment