Mshehereshaji
Bw. Salum Msellem kutoka Istiqama Radio akitambulisha meza kuu kwa
washiriki wa mafunzo ya Ujasiriamali ya siku moja kwa Vijana Visiwani
Pemba yaliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye ukumbi wa Shule ya
Sekondari Madungu.
Mratibu
wa YUNA kisiwani Pemba, Bw. Mohammed Ali, akisoma taarifa ya maendeleo
ya vilabu vya Umoja wa Mataifa visiwani humo na changamoto
zinazowakabili kwa walezi wa vilabu hivyo.
Na Mwandishi Wetu
Kituo
cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), kilifanya mafunzo yenye tija ya
ujasirimali kwa vijana katika Mji wa Pemba visiwani, Zanzibar na kupata
washiriki wenye kiu ya kutaka kujiajiri na kuondokana na umasikini hapa
nchini.
Akizungumza
kwenye uzinduzi rasmi wa mafunzo hayo ya siku moja ya ujasirimali kwa
vijana hivi karibuni Mjini Pemba, Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama amesema Umoja wa Mataifa
tangu mwaka 2000 walizindua malengo ya milenia ili kusaidia nchi
zinazoendelea kuondokana na umaskini.
“malengo
manane ya milenia ni pamoja na Afya ya Uzazi kwa kinamama, Elimu,
kuondoa umaskini na mambo ya mazingira vile vile kusaidia mikakati
mbalimbali ya nchi hizo katika utekelezaji wake mpaka kufikia mwaka
2015,” amesema Bi. Ledama.
Afisa
Vijana - Mshauri kutoka WIZARA ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya
Vijana, Wanawake na Watoto, Bi. Stara Salim akizungumzia jitihadi za
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuwawezesha Vijana kupata mikopo
kupitia asasi mbalimbali za fedha ili waweze kujikwamua kimaisha na
kuondokana na lindi la umaskini visiwani Pemba.
Amesema
kwamba kazi kuu ya Umoja wa Mataifa na taasisi zake ni kusaidia
Serikali mbalimbali katika nchi zinazoendelea kufanikisha mikakati na
utekelezeji wa malengo ya milenia ikiwemo dhana ya kupunguza umaskini.
Bi.Ledama
alilisitiza kwamba katika utekelezaji huo Umoja wa Mataifa inasaidia
mikakati hiyo ya kuondoa umaskini kwa kuandaa program mablimbali na
kufanya mafunzo ya ujasirimali kwa vijana ili waweze kujiajiri na
kuondokana na umasikini.
“Serikali
pekee haiwezi kutoa ajira kwa watu wote kwa sababu nafasi ni chache na
mahitaji ni makubwa kwa hiyo ndugu zangu kujiajiri na kuajiri wengine
katika sekta binafsi kupitia ujasirimali ni nafasi pekee ya kuondokana
na umaskini,” aliongeza.
Amesema
kwamba asilimia 43 ya wakaazi wa Zanzibar ni vijana kwa hiyo kuna
umuhimu mkubwa kwa Umoja wa Mataifa na sekta binafsi kuhamasisha
ujasirimali kama njia pekee ya kujiajiri na kuondokana na umaskini wa
kipato na wa jumla.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma
Ledama akizungumzia lengo la kuendesha mafunzo ya Ujasiriamali kwa watu
walio nje ya shule ikiwa ni moja ya agenda ya kutekeleza malengo ya
milenia ya kupunguza umaskini kwa nchi zinazoendelea.
Bi.
Ledama amesema sekta binafsi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo
wanaweza kupunguza tatizo la ajira kwa kusisitiza ujasirimali zaidi
katika maeneo mbalimbali ya Bara na Visiwani.
“Haya
ni mafunzo ya pili kufanyika bara na visiwani yenye kutoa mafunzo yenye
tija juu ya ujasirimali na faida zake katika kupunguza na kupambana
umasikini kwenye nchi zinazoendelea,” aliongeza.
Amesema
kwamba Shirika la Kazi Duniani (ILO) wana kitengo maalum cha mambo
kujenga uwezo kwa vijana na mafunzo ya ujasirimali yenye lengo la
kuondoa umasikini miongoni mwa vijana nchini Tanzania.
Mkufunzi
wa mafunzo ya Ujasiriamali kupitia Program ya kazi Nje nje inayolenga
kuelemisha Vijana stadi za Ujasiriamali iliyoasisiwa na Shirika la Kazi
Duniani (ILO) Bi. Mwanapili Hamad akitoa mada kuhusu dhana nzima ya
uongozi katika biashara (Business Management) kwa wajasiriamali Vijana
visiwani Pemba ili waweze kuboresha kipato chao.
Picha
juu na chini ni sehemu ya washiriki wa mafunzo ya Ujasiriamali ya siku
moja yaliyoratibiwa na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).
Mjasiriamali
mwenye kipaji cha kuchora ramani za majengo, kutengeneza sampuli za
nyumba kwa kutumia maboksi Bw.Steven Timothy Mihale kutoka Temeke Youth
Development Network (TEYODEN) akionyesha moja ya kazi zake kwa
wajasiriamali wenzake ambayo inampatia kipato na kuweza kuendesha maisha
yake.
Bw. Steven Mihale aliwapa moyo wajasiriamali wenzake na kuwataka kuwa na uthubutu na kutokata tamaa mapema.
Vijana wajasiriamali wakiangalia kazi ya Mjasiriali mwenzao.
Mmoja
wa washiriki wa mafunzo hayo akiuliza swali kwa wakufunzi wa mafunzo ya
Ujasiriamali yaliyoratibiwa na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC).
Mkufunzi
wa mafunzo ya Ujasiriamali Bi. Mgeni Salum akitoa somo la namna ya
kuhifadhi hesabu za mauzo na kujua kama biashara ina faida au hasara
sanjari na kupata mikopo kupitia taasisi za kifedha.
Mratibu
wa YUNA kisiwani Pemba, Bw. Mohammed Ali akiteta jambo Mkutubi wa Kituo
cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Harriet Macha (katikati)
wakati wa mafunzo ya Ujasiriamali kwa vijana visiwani Pemba
yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Madungu.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma
Ledama, akifunga mafunzo ya siku moja ya wajasiriamali Visiwani Pemba
yaliyoratibiwa na kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).
Post a Comment