Kundi
la wahamiaji haramu zaidi ya 40 wanaodhaniwa kuwa ni wa kutoka Ethiopia
na Somalia wakishuka kwenye Lori aina ya fuso katika kituo kikuu cha
muda baada ya kukamatwa wilayani Same wakijiandaa kusafirishwa kwenda
nchi ya Afrika kusini.
Gari aina ya Fuso lililokutwa likiwa limebeba wahamiaji haramu tayari kuwasafirisha kwenda Afrika kusini.
Wahamiaji
haramu wakiwa katika ofisi za kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro
muda mfupi baada ya kufikishwa wakitokea wilayani Same ambako walikutwa
wakijiandaa kutaka kusafirishwa kwenda Afrika kusini.
----
Na Dixon Busagaga,Moshi.
WAHAMIAJI
haramu 56, Raia wa nchini Ethiopia, wamekamatwa katika Kijiji cha
Jiungeni, Kata ya Ruvu, wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, Ofisini Kwake, Kamanda wa Polisi mkoani
Kilimanjaro, Robert Boaz alisema Wahabeshi hao walikamatwa majira ya saa
sita usiku, usiku wa kuamkia Juzi, wakiwa katika Lori aina ya Fuso,
yenye namba za usajili, T188 AYU, mali ya kampuni ya E.Lyimo ya Mjini
Moshi.
Kamanda
Boaz alisema baada ya kupata taarifa ya uwepo wa watu wanaotiliwa
mashaka kijijini hapo, polisi walianza kufuatilia na kuwahi Gari hilo
likiwa na Wahamiaji hao ambao hata hivyo bado haijafahamika walikuwa
wakielekea wapi.
“Polisi
waliwahi baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi na kukamata
wahabeshi 56, walikuwa wanasafirishwa kwenye Lori aina ya Fuso, namba za
usajili T188 AYU mali ya E.Lyimo ya mjini Moshi, bado hatujafahamu
walikuwa wanaelekea wapi lakini uchunguzi unaendelea,” alisema Boaz.
Kamanda
Boaz alisema mbali na Wahabeshi hao 56, Polisi walifanikiwa kuwakamata
Watanzania Watatu akiwemo Dereva wa Lori hilo, aliyetambulika kwa jina
la Daniel Mfinanga pamoja na wenzake wawili ambao majina yao
yanahifadhiwa kutokana na sababu za kiupelelezi.
Aidha
Kamanda Boaz aliongeza kuwa Utingo wa Lori hilo, aliyemtaja kwa jina la
Ismael Juma, alifanikiwa kutoroka na kwamba jeshi hilo kwa sasa
linaendelea na msako ili kumtia mbaroni.
Post a Comment