Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili zima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu. SAMAHANI KWA PICHA UTAKAZOZIONA |
Muuguzi
wa zamu Bi. Neema Bayo akimfunika majeruhi Bi. Neema Teti aliyemwagiwa
maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu. SAMAHANI KWA PICHA UTAKAZOZIONA
|
Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu. SAMAHANI KWA PICHA UTAKAZOZIONA |
Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili zima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu. SAMAHANI KWA PICHA UTAKAZOZIONA |
Na Gadiola Emanuel -Arusha
Mwanamke
mmoja mkazi wa Mbuguni Arusha,Bi. Neema Teti amejeruhiwa vibaya kwa
kumwagiwa maji ya moto katika sehemu mbalimbali za mwili wake katika
kisa kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi. Tukio hilo limetokea baada ya
mtekelezaji wa kitendo hicho Mama Tatu Msuya ambaye ni jirani yake
akidaiwa kumtuhumu majeruhi huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume
wake.
Katika wodi ya wagonjwa majeruhi hosipitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru
alikolazwa,Neema ameelezea tukio hilo kuwa limetokea juma lililopita
baada ya kuitikia mwito wa jirani yake Tatu Msuya uliomtaka afike
nyumbani kwake kwaajili ya kumsaidia uangalizi wa familia yake kutokana
na kuhitajika msibani na ndipo alipomjeruhi vibaya kwa kumwagia maji ya
moto.Neema Teti-Majeruhi
Muuguzi wa zamu katika hospitali ya Mount Meru,Neema Bayo amesema
majeruhi huyo aliletwa hospitalini hapo akiwa katika hali mbaya lakini
hali yake imezidi kuimarika baada ya kupatiwa matibabu na jopo la
madaktari hospitalini hapo. Nae Muuguzi wa wodi ya majeruhi mount Meru
Hospitali Bi.Neema Bayo amesema matukio kama hayo yakizidi kushamiri katika maeneo mbalimbali nchini,bado inaelezwa kuwako kwa ugumu wa kutoa taarifa katika vyombo vya sheria kutokana na wahusika kuwaficha wahalifu mara wanapotoka hospitalini
Afisa wa dawati la jinsia mkoa wa Arusha Maria Maswa akizungumza
wakati alipotembelea waathirika wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia
katika
hospitali ya mount Meru,amesema yanapotokea matukio hayo,walengwa
wamekuwa wagumu kutoa ushirikiano kwa madai ya kumaliza swala hilo
kinyumbani hatua inayochochea ukuaji wa matatizo hayo.
Maria Maswa-Afisa Dawati la Jinsia Mkoa wa Arusha Bi. Maria Maswa alisema "Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limeeleza kuwa linaendelea na msako dhidi ya Mama Tatu Msuya anayedaiwa kutekeleza kitendo hicho; pia aliongeza kuwa jumla ya kesi 507 zimeripotiwa kati kipindi cha mwezi november 2012 mpaka sasa. Picha zote na Gadiola Emanuel wa Wazalendo 25 Blog.

Post a Comment