SIKU
chache baada ya gazeti dada na hili la Amani kuandika habari ya mtoto wa
miaka 7, Sara Shija kuilea familia bila msaada wa wazazi wake, mambo
mazito zaidi yamefichuka.
Mara
baada ya taarifa za habari hiyo kutapakaa mitaani, imebainika kwamba
baba mzazi wa familia hiyo inayoishi Bangulo, Kata ya Pugu amefungwa.
Risasi
Mchanganyiko limeongea na mjumbe wa eneo wanaloishi watoto hao, Juma
Kabuwa ambaye alithibitisha kufungwa kwa mzazi wa watoto hao aitwaye
Shija.
“Baba yao
alipoondoka nyumbani alikwenda Kibaha Maili Moja, huko kwa rafiki yake
akakutana na mgogoro wa kugombea shamba ndipo alipofungwa jela,” alisema
mjumbe huyo.NA GPL
Akifafanua
zaidi, mjumbe huyo alisema bwana Shija alienda Kibaha kwa rafiki yake
ambaye ndiye aliyekuwa kwenye mgogoro huo wa shamba na yeye akaingia
kumsaidia ndipo alipokamatwa na polisi na kuwekwa ndani.
Mjumbe huyo alisema kuwa taarifa hizo alizipata…
Post a Comment