Baadhi
ya wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wakimsikiliza Mwenyekiti wa
Chama hicho Professa Ibrahim Haruna Lipumba katika uzinduzi wa kampeni
za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki katika kiwanja cha Bustani
ya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi Unguja.Mwenyekiti
wa Chama cha Wananchi (CUF) Professa Ibrahim Haruna Lipumba na viongozi
wengine wa chama hicho wakirusha maputo kama ishara ya uzinduzi wa
kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki uliofanyika Bustani
ya Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi Unguja.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wananchi (CUF) Professa Ibrahim Haruna Lipumba akimnadi
mgombea wa Chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki,
Abdulmalik Haji Jecha, katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa
Jimbo la Kiembesamaki zilizofanyika Bustani ya Kiembesamaki, Wilaya ya
Magharibi Unguja.Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar.
Na Miza Kona – Maelezo
Mwenyekiti
wa chama cha Wananchi CUF Taifa Profesa Ibrahim Haruna Lipumba
amewataka wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki kumchagua kiongozi
atakayeweza kuingia katika bunge la katiba na kuyatetea na kuleta
maslahi ya Zanzibar.
Kauli
hiyo ameitoa jana huko Kiembesamaki wakati alipokuwa akizindua kampeni
na kumtambulisha mgombea uwakilishi kupitia chama hicho.
Amesema
kiongozi bora ni yule atakaeweza kuitetea Zanzibar na kuipatia
maendeleo na kupata mamlaka yake kamili pamoja na kuleta mabadiliko.
Aidha ameeleza kuwa CUF inataka kuleta mabadiliko katika mambo ya muungano na kuona kuwa haki inafanyika katika nchi zote.
Aidha
amesema kupita chama cha CUF wananchi watapata kiongozi mzuri
atakaeweza kuingia kwenye bunge la katiba na kuitetea nchi bila ya woga
wala kupoteza mwelekeo.
“Mpeleke mtu atakaeweza kuingia kwenye bunge la katiba na kutetea maslahi ya Zanzibar”, alifahamisha.
Hata hivyo amesisitiza kuwa uchaguzi ufuate utaratibu uwe huru na haki bila ya kushirikisha vyombo vyengine.
Nae
mgombea uwakilishi AbdulMalik Haji Jecha amesema pindipo wananchi
watamchagua ataitetea Zanzibar kwa moyo wa uzalendo na kuleta maendeleo
kwa maslahi ya nchi.
Uchaguzi
huo mdogo wa jimbo la Kiembesamaki unafanyika kutokana na aliyekuwa
mwakilishi wa Jimbo hilo Mansour Yussuf Himid kuvuliwa uwanachama
kupitia CCM
Post a Comment