 |
| PC David Alfred |
Akizungumza na waandishi wa habari leo
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangala amesema tukio
la askari wake aitwaye David Alfred (25-30)kujeruhiwa kwa risasi
limetokea jana majira ya sa 12 na nusu jioni wakati askari huyo akikagua
silaha aina ya SMG katika ghala la silaha katika kambi ya jeshi la polisi mjini Shinyanga ili aingie kazini.
 |
| Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga akizungumza na waandishi wa habari mapema leo kuhusu tukio la askari kujeruhiwa kwa risasi |
Amesema wakati askari huyo akikagua
silaha hiyo ghafla risasi ilifyatuka na kumjeruhi chini ya bega la mkono
wa kushoto hali iliyopelekea akimbizwe katika hospitali ya mkoa wa
Shinyanga kwa ajili ya matibabu.
Amesema tukio hilo ni bahati mbaya tu
huku akiwataka askari polisi kuwa makini na kujali usalama wao kwanza
kabla na wakiwa kazini.
 |
Dkt Fredrick Mlekwa akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya mkoa
Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa amesema hali ya majeruhi huyo inaendelea
vizuri anaongea, vizuri na kwamba kufuatia tukio hilo askari huyo amepata majeraha katika sehemu za kifuani na mkono wa Kushoto.
|
on Tuesday, January 7, 2014
Post a Comment