Wanaotuhumiwa kwa ujambazi wa kutumia siraha
HAKIMU
Mkazi wa Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Michael Mteite
amewagiza wakili kuhakikisha anampeleka mtuhumiwa mahakamani hata kwa
machela.
Hakimu Mteite alilazimika kutoa kauli hiyo wakati akisikiliza kesi inayowakabili Askari wawili wa jeshi la
Polisi na Magereza pamoja na watu watatu ambao ni raia wa kawaida wanaotuhumiwa kwa ujambazi wa kutumia silaha.
Kauli ya
Hakimu ilikuja kufuatia mmoja kati ya washtakiwa wote watano kushindwa
kuhudhuria mahakamani wakati kesi yao ilipangwa kuendelea na ushahidi
baada ya Wakili wa Serikali Archiles Mulisa kuhoji Mhakamani kuwa
Mshtakiwa namba mbili Elinanzi Mshana(22)Mkazi wa Iyela Jijini Mbeya
hajafika huku upande wa jamhuri ukiwa hauna taarifa.
Kutokana
na hoja hiyo ndipo aliposimama Wakili wa Utetezi ambaye anawasimamia
watuhumiwa wote wato, Ladislaus Lwekaza na kuiambia Mahakama kuwa
Mshtakiwa namba mbili ameshindwa kuhudhuria kesi yake kutokana na kuwa
majeruhi yaliyotokana na kupigwa risasi sehemu ya paja hivyo kumfanya
kuwa na maumivu makali anayougulia akiwa gerezani.
Lwekaza
alidai kuwa kutokana na mteja wake huyo kuwa majeruhi aliiomba mahakama
kuahirisha kesi hiyo hadi hapo mtuhumiwa huyo hali yake itakapotengemaa
na kuongeza kuwa pia hawataweza kuendelea na kesi kutokana na washtakiwa
wote kutopewa hati za mashtaka na maelezo ya mlalamikaji ili wajiandae
na utetezi.
Hata
hivyo Wakili wa Serikali Mulisa alisimama na kumuuliza Wakili wa utetezi
kuwa anapaswa kuiambia mahakama kifungu alichotumia kudai hati ya
mashtaka pamoja na maelezo ya mlalamikaji sambamba na majeraha aliyopata
mtuhumiwa kuwa aliyapata wakati gani na lini.
Kwa
upande wake Hakimu Mteite aliiambia Mahakama kuwa kutokana na ubishani
wa pande zote mbili ameona aingilie na kuwashauri kuwa madai ya upande
wa utetezi kuhusu hati ni haki ya kikatiba kupewa mshtakiwa.
Mteite
aliongeza kuwa madai ya majeruhi ya Mshtakiwa namba mbili ni mbinu za
kuchelewesha kesi ambazo mara nyingi hufanyika ili mahakama ishindwe
kuendelea na kesi na kuongeza kuwa yeye binafsi pamoja na mahakama
hakubaliani na suala hilo.
Alisema
kama taarifa za ugonjwa huo zingikuwa za kweli Jeshi la Magereza linajua
taratibu ambapo mgonjwa hupelekwa Hospitali ambapo mahakama ikitambua
huhamishia kesi zake hospitali.
Alisema
Wakili wa utetezi anapaswa kutambua kuwa mwenendo wa Mahakama wa siku
hizo tofauti na zamani ambapo kesi moja ilikuwa ikichukua hadi zaidi ya
miaka mitatu lakini sasa wamejipanga kumaliza kesi mapema kabisa.
Kutokana
na hali hiyo Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 20 Mwaka huu na
kumwagiza Wakili wa Utetezi Lwekaza kuhakikisha inampeleka Mtuhumiwa
siku ya kesi kwa njia yoyote hata kama ni mgonjwa namna gani ikiwa ni
pamoja na kumbeba kwa machela au gari la wagonjwa.
Pia
alimwagiza mwendesha mashtaka wa Serikali kuhakikisha anawapatia
washtakiwa madai yao ambayo ni kupatiwa hati za mashtaka, nakala ya
maelezo ya mlalamikaji pamoja na mwenendo wa awali wa kesi.
Awali
Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa akisaidiwa na Basilius
Namkambe alisema washtakiwa wote kwa pamoja wanatuhumiwa kwa kosa moja
la unyang’anyi wa kutumia Silaha kinyume cha Sheria kifungu cha 287 sura
ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Mulisa aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mshitakiwa namba moja ambaye ni Askari Polisi PC James mwenye
namba F8302 wa Wilaya ya Mbeya ambaye kabla ya kufikishwa mahakamani alivuliwa Uaskari baada ya kuhukumiwa kijeshi.
Aliwataja
wengine kuwa ni mshtakiwa namba mbili kuwa ni Elinanzi Mshana(22)Mkazi
wa Iyela Jijini Mbeya, Askari Magereza mwenye namba B 500 Sajenti Juma
Mussa(37) wa Gereza la Ruanda Mbeya,Mbaruku Hamis(29) Mkazi wa Iyela na
Amri Kihenya(38) Mkazi wa Iyela.
Akisoma
mashtaka yao Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite,
Mulisa alisema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Januari 3, Mwaka huu
majira ya saa 11 jioni katika eneo la Mlima Kawetere barabara ya Mbeya
Chunya.
Alisema
watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kulizuia gari aina ya
Pick Up lililokuwa likiendeshwa na Ezekia Matatira (34) Mkazi wa Iyunga
Jijini Mbeya
ambaye
alikuwa na mtu aliyekuwa akifahamika kwa jina la Sreedhar Pasupelet(38)
mwenye asili ya Kiasia wakitumia magari madogo mawili ambayo ni GX 100
Toyota Cresta T 782 BEU na Gari linguine ambalo lilikuwa na namba za
Chesesi GX 6011832 AINA YA Grand Mark II.
Na mbeya yetu
Post a Comment