TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Taasisi mbali mbali za kijamii, vyama vya kitaaluma na
vyama vya siasa vipatavyo 50 hadi leo, Jumanne,
Desemba 31, 2013, vimewasilisha majina ya watu wao
ambao vinapendekezwa wafiriwe katika kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
Taarifa iliyotolewa leo mjini Dar Es Salaam na Katibu
Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue inasema
kuwa taasisi hizo zimewasilisha majina yao kwa
mujibu wa mwaliko uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa makundi yaliyobainishwa katika Kifungu
cha 22(1) (c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba (Sura
ya 83).
Taarifa hiyo imesema kuwa makundi hayo 50
yaliyowasilisha majina yanayopendekezwa kwa ajili ya
uteuzi yanatokana na barua 169 zilizopokelewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Sefue na Ofisi ya
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi,
Zanzibar.
Makundi
ambayo yamewasilisha majina ni yafuatayo: Shirika la Wasaidizi wa Jamii
Kabila la Wagogo, Tanzania Association of Social Workers (TASOWA),
Teachers and Student Forum Tanzania, Tanzania Women Teachers
Association, Umoja wa Wanawake Wajane Wilaya ya Karagwe na Kyerwa (UWK),
Tanzania Peace and Development Society, Better World Organization
(BWO), Youth Focus and Development, Association of Traditional Medicine
Man, Registered Centre for Good Governance and Development in Tanzania,
Chama Cha Kijamii (CCK), CHANETA na Muungano wa Wanajeshi Wastaafu
Tanzania. Makundi mengine ni Legal Aid Iringa Village, Tanzania Kilolo
Orphans and Social Development Organization, Legal aid and Social
Welfare Association, Legal and Human Right Centre, Tanzania Lift
Initiative NGO, Kilolo Paralegal Unit, Women Development and Social
Activities Association, Defence of Human Right/Citizen Rights, DAWSEN
Trust Fund, Baruti Development Association (BADEA), Living Hope
Ministries Trust, EFATHA Ministry, Bethel Assemblies of God Tanzania,
Muslim and Christian Brotherhood Society, Baraza Kuu la Waislamu wa
Kondoa – Tanzania na Jesus Temple Inner Transformation News. Taasisi
nyingine ni Jumuiya ya Waithna Asharriyyah Tanzania, Rehmatfi Sabilillah
Trust of Tanzania, Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), National
Reconstruction Alliance (NRA), Sauti ya Umma (SAU), Chama cha Demokrasia
Makini, African Progressive Part – APPT Maendeleo, National League for
Democracy, Tanzania Film Federation, Taasisi ya Maendeleo ya Utamaduni,
Al-Amoud General Enterprises, Blue Belt and Water Sources Control,
Community Development Training Institute – Tengeru, Tanzania Medical
Student Association, Tanzania Sea Farmers Union, Medical Association of
Tanzania, Chama cha Wastaafu wa Mbinga, Union of Tanzania Press Clubs,
Umoja wa Wanawake Tanzania, Alliance for Tanzania Farmers Party,
Tanzania Social Economic and Environment and Wellbeing. Kwa vile mwisho
wa kupokea orodha ya majina hayo
ni tarehe 02 Januari, 2014, Balozi Sefue ametoa mwito
kwa makundi mengine ambayo hayajawasilisha
orodha hiyo kufanya hivyo kabla muda uliowekwa
kuisha. Aidha, wakati wa kuwasilisha ni muhimu
kuzingatia vigezo vilivyowekwa na sheria na kama vilivyofafanuliwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 443
lililochapishwa tarehe 13 Desemba, 2013. Vilevile ni
muhimu kuzingatia kuwa majina yanayopendekezwa
na Taasisi au makundi yaliyoainishwa kwenye sheria
na siyo mtu binafsi kujipendekeza mwenyewe.
Kwa wale watakaojipendekeza wenyewe wajue kuwa watakuwa wanakwenda kinyuma na maelekezo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Desemba, 2013
Post a Comment