Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

IRINGA WAMBEBESHA MZIGO WAZIRI MGIMWA HATA KABLA YA KUAPISHWA KWAKE




 Mbunge Mgimwa ambae ameteuliwa  kuwa naibu  waziri wa maliasili na utalii akizungumza na wapiga kura   wake jimboni


Mbunge wa  Mufindi kaskazin Mahmood Mgimwa  kulia akiwa na mbunge wa Mufindi kusini Mendrady Kigolla na mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu kushoto katika kikao cha uteuzi wa wanafunzi  wa waliofaulu  kuingia kidato cha kwanza mwaka  huu.(picha na Francis Godwin Blog)




BAADA  ya  Rais Jakaya  Kikwete  kufanya mabadiliko ya baraza la  mawaziri  ikiwa ni pamoja na  kuteua sura mpya  za   mawaziri na  manaibu  kuingia katika baraza  hilo  wananchi  wa  jimbo la Mufindi kaskazin wamempongeza  mbunge wao Mahmood Hassan Mgimwa kwa  kuteuliwa  kuwa naibu waziri wa maliasili na utalii na  kumwomba pindi atakapoapishwa  kuanza  kazi ya  kufuatilia orodha  ya vibali  vya vitalu vilivyotolewa na wizara  ya maliasili na utalii ili kuona kama haki imetendaka katika utoaji wa  vibali  hivyo.



Wakizungumza kwa nyakati  tofauti na mtandao huu wa www.matukiodaima.com  katika mahojiano maalum baada ya  uteuzi huo  leo  walisema  kuwa  wanampongeza Rais Kikwete kwa  kumteua mbunge wao kuwa katika baraza  hilo na kutokana na mbunge huyo awali kabla ya nafasi hiyo kuonekana ni mwenye shauku ya  kusaidia  wapiga kura  wake katika maendeleo na kero mbali mbali ikiwemo ya vibali ni wazi ataitumia nafasi hiyo  kuweka  uwiano mzuri katika utoaji wa vibali vya vitalu katika msitu  huo wa Taifa wa Sao Hill Mufindi.



JOhn Kalinga mkazi  wa Mafinga  alisema  kuwa  kilio   kikubwa  cha wana Mufindi ni juu ya upendeleo ambao  umekuwa  ukifanywa  katika  utoaji wa vibali ambapo  baadhi ya  watu  wamekuwa  wakipewa vibali  zaidi ya  kimoja kwa  kutumia majina  tofauti jambo ambalo  linawanyima haki wasio na  uwezo wa kufanya  hivyo.



Kwani  alisema mbali ya  kuwa  mwaka huu vibali  hivyo  vimetolewa juzi  ila wapo  baadhi ya  watu  wamepewa kibali  zaidi ya kimoja na  kuwa  suala  hilo  wanaomba Mgimwa  kuweza  kufuatilia  hasa  ukizingatia msitu  huo upo  jimboni  mwake kwa  asilimia  kubwa  zaidi na jimbo la Mufindi kusini kwa kiasi .



Hata   hivyo  alisema  imani ya  wana  Mufindi kwa baraza  hilo  ni kuona linafanya kazi  zaidi na wananchi ili  kuweza  kumsaidia  Rais Kikwete kumaliza muda  wake  vizuri na  CCM kuendelea  kubaki madarakani .



Matrida  Sanga  mkazi  wa kinyanambo Mafinga  alisema   kuwa  Rais  Kikwete hajakosea  kumteua  Mgimwa  kuunda  baraza la mawaziri  kwani ni  mmoja kati ya  wabunge  wanaojituma  sana katika  kutumikia Taifa.



Japo  alisema imani  ya  wananchi wa Mufindi  kwake ni  kuona kero  ya  wananchi wa mji wa Mafinga  inayotokana na ucheleweshaji wa utoaji wa vibali  vya uvunaji mbao  katika msitu  wa Sao Hill  na  upendeleo unakomeshwa  ili  kuepusha  vijana kuingia  mitaani kukaba  watu kwa kukosa ajira.



Katibu  mwenezi  wa Chama  cha mapinduzi (CCM)  wilaya ya Mufindi Daud Yassin alisema  kuwa  wao kama  chama  wanampongeza Rais Kikwete kwa  kumteua  mbunge  wao  kuingia katika baraza hilo  kwa  ni heshima kubwa katika wilaya ya  Mufindi ambayo imepata  .



" Kwanza utambue kuwa  mimi ni katibu  mwenezi wa CCM wilaya  na   Mgimwa na mbunge  wangu kati ya   wabunge  wawili  tulionao katika  wilaya ya Mufindi ....hivyo  kuteuliwa kwake ni  heshima  kubwa katika  chama  na kwa wakazi wa  wilaya  nzima ya  Mufindi na mkoa  wa Iringa"


Hata  hivyo  alipoulizwa  kuhusu  kero ya   wananchi  juu ya vibali  vya uvunaji  miti  katika msitu  wa Sao Hill Yassin alisema kwa  sasa hayupo tayari  kuzungumzia  hilo kwa sasa anapewa  pongezi  zake  kwanza .
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top