HERUFI A
Mwenye jina linaloanziana na herufi A
ni mtu anayependa mambo
makubwa, anajiamini na mwenye
uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni
mtu mwenye tahadhari, mchangamfu
na mpenda matukio. Anapenda
Kuheshimiwa, anapenda Mamlaka, na
ana kiburi, na hasira.
HERUFI B
Mwenye jina linaloanziana na herufi B
ni mtu, mkarimu, muaminifu, na
hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na
mkatili katika vita au pale anapotaka
kulinda vilivyo katika himaya yake.
HERUFI C
Mwenye jina linaloanziana na herufi C
ni mtu wakubadilika badilika,
mshindani na hupenda kupigania
malengo yao wanayopenda. Ni watu
wa wabunifu na wanaopenda
mawasiliano
HERUFI D
Mwenye jina linaloanziana na herufi D
ni mtu anayependa usawa, Biashara.
Ni watu wanaopenda kuamrisha na
mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na
wenye msimamo.
HERUFI E
Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni
mtu mwenye roho nzuri
yenye mapenzi na huruma. mwenye
kupenda uhuru katika mapenzi na
mchangamfu. Kinyume na hivyo
atakuwa ni mtu asiotegemewa na
kigeugeu.
HERUFI F
Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni
mtu mwenye mapenzi,huruma , roho
nzuri na ana uwezo wa kuwafariji
watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye
huzuni lakini ni mzito wa kufanya
maamuzi.
HERUFI G
Mwenye jina linaloanzia na herufi G ni
mtu mwenye mwenye imani ya kidini
na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha
kubuni na uwezo wa kutatua matatizo
ya watu. ni mtu mwenye hisia
kali,msomi, mpweke na mkaidi wa
kukubali ushauri wa kutoka kwa watu.
HERUFI H
Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni
mtu mwenye ubunifu na nguvu katika
biashara, hupata faida kubwa
kutokana na jitihada na bidii zake. ni
mwenye mawazo mengi, mchoyo na
mbinafsi.
HERUFI I
Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni
mtu mwenye kupenda sheria, ana
huruma na utu. Wakati mwingi
hajiamini na ni mwenye hasira za
haraka.
HERUFI J
Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni
mtu mwenye matamanio,mkweli,
mkarimu na muerevu. asiyekubali
kushindwa na hupata mafanikio
makubwa. Wakati mwingine anakuwa
ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo.
HERUFI K
Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni
mtu mwenye jeuri, mwenye
msimamo thabiti,mashuhuri na
mwenye uwezo wa kushawishi na
kuamsha hisia za watu wana uwezo
wa utambuzi ambao watu wengi
hawana. Ni mtu asioridhika na hali ya
kimaisha.
HERUFI L
Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni
mtu wa vitendo, mwenye hisani na
aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa
wanapata ajali mara kwa mara.
HERUFI M
Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni
mtu mwenye kujiamini sana,
mchapakazi na hupata mafanikio. ni
mtu mropokaji,mwenye haraka na
mwepesi kukasirika.
HERUFI N
Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni
mtu mwenye ubunifu, hisia kali na
hupenda kuwasiliana lakini ana wivu
sana.
HERUFI O
Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni
mtu mwenye subra, mvumilivu na
mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu
mwenye kupenda kutumikia jamii na
mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti
hisia.
HERUFI P
Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni
mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na
hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho
lakini anapenda sana kujitumbukiza
kwenye mambo ya watu.
HERUFI Q
Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni
mtu mwenye kupenda mambo ya
asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana
uwezo wa kuonyesha vitu
visivyojulikana hata hivyo ni mtu
aliyepooza sana.
HERUFI R
Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni
mtu mwenye uvumilivu, wenye
huruma lakini ana hasira za haraka.
Muda wote anakuwa mpenda amani.
HERUFI S
Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni
mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta
utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya
ghafla na hupenda mageuzi
makubwa.
HERUFI T
Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni
mtu mwenye kupenda ushauri wa
kiroho, anatumia nguvu za ziada
kusaidia watu na hupata mafanikio
baada ya muda mrefu. Ni watu wenye
hisia kali sana na ni wepesi
kushawishika.
HERUFI U
Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni
mtu mwenye bahati kubwa kwa
ujumla. Anapenda uhuru katika
mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi,
mwenye tamaa na aliyekosa
maamuzi.
HERUFI V
Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni
mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie
choka. Hata hivyo ni watu
wasiotabirika.
HERUFI W
Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni
mtu muwazi, wachangamfuu kupita
kiasi na mwenye uwezo wa kutambua
mtu mwema na mbaya. Ni watu
wenye tamaa na hufanya mambo ya
hatari.
HERUFI X
Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni
mtu asiyependa kuwekewa vizuizi
katika kwenye anasa na ni rahisi
kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa
uaminifu. Herufi X inawakilisha Nyota
ya Samaki.
HERUFI Y
Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni
mtu mwenye kupenda Uhuru na
hawapendi kupingwa jambo lao
lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na
husababishia kupoteza bahati katika
maisha.
HERUFI Z
Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni
mtu mwenye kupenda matumaini na
amani. Ni wenye msimamo mkali ila
wanashauriwa kufikiria kabla ya
kuamua jambo.
on Thursday, January 16, 2014
Post a Comment