Katibu
tawala Mkoa, Mkuu wa mkoa Kagera Mh. Fabian Massawe, Naibu Waziri wa
TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Ludovick Utouh
wakiingia ukumbini leo Bukoba.
Mkuu
wa mkoa Kagera Mh. Fabian Massawe, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey
Mwanri na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoka Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Bw. Ludovick Utouh
Mkuu
wa mkoa wa Kagera Mh.Fabian Massawe akimkaribisha mgeni Rasmi leo
kwenye kikao hicho cha kukamilisha Ukaguzi Maalum" Exit Meeting" Cha
mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali leo Januari 17.2014 Mjini
Bukoba ambapo kikao hicho kilianza mapema saa 5 Asubuhi.
Taswira Ukumbini
Meya
wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani (kulia) pamoja na Madiwani wa
Manispaa ya Bukoba ambapo swala kubwa kwa Madiwani....wanamtuhumu ndugu
yao Meya kwa matumizi mabaya ya madaraka.Mkurugenzi mpya wa manispaa ya bukoba Ambekiswe shemwela
Naibu
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Ludovick
Utouh (kulia) ambaye alikuwa ni mwakilishi wa Waziri Mkuu, akiteta jambo
na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw. Fabian Massawe katika Meza kuu.
Bw.
Ludovick Utouh ameambatana na Bw. Mero, Bi Mwadawa A. Mgendera na Bw.
Elisha M. Nkwija pamoja na Bw. Sabuni ambao wameshiriki kufanya ukaguzi
Bukoba Mjini.
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoka Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Bw. Ludovick Utouh akitoa taarifa ya ukaguzi maalum leo
Bukoba.
Naibu
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri (katikati) ambaye pia
alimwakilisha Waziri mkuu akimsikiliza kwa makini Bw. Ludovick Utouh
Viongozi wakifuatilia kwa makini
Viongozi Meza kuu wote walikuwa makini kusikiliza taarifa hiyo Muhimu ya Ukaguzi.
Bw. Ludovick Utouh akiendelea kutoa Taarifa ya Ukaguzi maalum leo
Taswira ya kikao chenyewe ndani
Waheshimiwa
Madiwani wa Manispaa ya Bukoba kulia ni Mstahiki Meya Anathory Amani
ambaye madiwani wa manispaa wanamtuhumu kwa matumizi mabaya ya madaraka.
CAG akiendelea na kazi!
Furaha hapa!!
Mkurugezi wa Manispaa Bukoba( kulia) Bw.Limbakisye Shimwela
Mkurugezi wa Manispaa Bukoba (kulia) Bw. Limbakisye Shimwela akiwa na viongozi wengine wakisikiliza taarifa ya ukaguzi leo
Taswira Ukumbini leo wakati wa kikao cha kukamilisha Ukaguzi maalum Mkoani hapa Kagera
Mstahiki
Meya Anatory Amani (kulia) kushoto ni Mzee Rwangisa, Ukumbuke pia Mzee
huyo Rwangisa ndiye aliyemwachia nafasi Meya Anatory Amani.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri ndie aliyemalizia kwa kutoa Maelezo ya Serikali.
Baadhi ya Madiwani wakisikiliza kwa makini.
Naibu
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akiendelea kutoa Maelezo ya
Serikali. Kuhusu Suruhisho hilo ambapo yamebainika Makosa ya Meya
Anatory kufanya makubaliano bila idhini ya Madiwani na Taratibu za
serikali, Basi ajipime Mwenyewe na Kujiudhuru mara moja kwa Maslahi ya
Manispaa ya Bukoba.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akiendelea kutoa maelezo ya serikali kiujumla na kukamilisha ukaguzi huo.
Watumishi wa Manispaa wachukuliwe hatua
Bw. Khamis Kaputa avuliwe Madaraka
Mhandisi,Mweka hazina nk wapoteze vyeo vyao!
Wakandarasi wote waliopata fedha bila taratibu wazirejeshe.
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Mh.Fabian Massawe (kulia) akisikitika baada ya
kumsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri ambaye
aliyemwakilisha vyema Waziri Mkuu.
Katibu Tawala wa Mkoa Kagera Bw. Nassor Mnambila kushoto nae akisikitika leo kwenye "Exit Meeting"
**Muda mfupi baadae uliopita Meya ametangaza kujiuzulu nafasi yake baada ya ripoti ya CAG kusomwa na kubaini mapungufu makubwa**
Post a Comment