Msafara wa mgombe udiwani kwenda kuchukua fomu uwanja wa nanenane zilipo ofisi za Msimamzi wa uchaguzi
MGOMBE
Udiwani kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro kwa tiketi ya Chadema Juma
Tembo juzi amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa mbwembwe baada ya
kusindikizwa na msafara wa magari na pikipiki.
Kata ya
Tungi imeingia kwenye uchanguzi mdogo baada ya aliyekuwa diwani wa kata
hiyo Mh Daud Mbao'CCM' kuiaga dunia na tume ya uchanguzi kuandaa
uchaguzi mdogo kuziba nafasi ya marehemu huyo aliyeugua kwa muda mrefu
muda.
Mgombe huyo akiwasili ofisi za msimamizi wa uchanguzi
wapambe wake wakishuhudia
Akiwasili ofisi zaChadema kata ya Tungi
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi hiyom ya kata baada ya kuchukua fomu
Wakishangilia nje ya Ofisi hiyo ya kata
Akisaini baada ya kuchukua fomu hiyo
Wakiondoka baada ya kuchukua fomu
ambapo walipita nyumbani kwa mgombe udiwani kwa tiketi ya CCM jirani na
ofisi za kata za Chama hicho
Chama cha
Demokrasia na Maendelea'CHADEMA' kimemteua Juma Tembo aliyegombe ubunge
jimbo la Morogoro Kusini 2010 na kushindwa na mpinzani wake mkubwa
lnnocent Kalogerezi'CCM' ameteuliwa tena na chama chake kugombe udiwani
katika kata hiyo.
Juzi
Diwani huyo alikwenda kuchkua fomu na msafara mkubwa wa magari na
pikipiki akitokea ofisi za wilaya za Chama hicho zilipo mtaa wa Konga na
kuelekea kata ya Tungi umbali wa takribani kilometa 12 kwenda kuchukua
fomu hiyo.
Baada ya
kukabidhiwa fomu hiyo na msimamizi msaidizi wa uchnguzi huo Bw Abuu
Rashid Liwangila alimkabidhji pia kitabu cha kanuni za uchanguzi huo.
Akizungumza
na Mtandao huu Msimanizi huyo alisema zoezi la uchukuaji fomu lilianza
Januari 2 na mwisho wa kurejeshwa fomu hizo ni January 15.
"Baada ya
zoezi hilo kukamilia kampenzi za uchaguzi huo zitaanza Januari 16 na
kufikia tamani Februari 8"alisema Bw Liwangila ambaye pia ni Afisa
Mtendaji wa kata hiyo ya Tungi.
Msimamizi
huyo amedai kwamba mpaka sasa ni wagombea wawili ndio waliofuika
ofisini wake na kuchukua fomu hizo ambapo alipotakiwa kuwataja wagombe
hao na vyama vyao Afisa Mtendaji huyo aligombe.
Pekua
pekua ya Mtndao huu imebani wagombe hao ni wavyama vya CCM na Chadema
ambapo CCM imemsimami mwanamke aliyefahmika kwa jina la Mama Twaha
Manispaa ya Morogoro inajumla ya kata 29 na kata zote zinaongozwa na madiwani wa chama cha Mapinduzi'CCM'
Post a Comment