Mwili wa Marehemu Milembe Jengamalulu ukiwa eneo la tukio |
Mwanamke mmoja Alifahamika kwa jina la Milembe Jengamalulu anayekadiriwa kuwa na umri
wa miaka 50-55, mkazi wa Ulowa no 4 wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga
umri wa miaka 50-55, amefariki dunia baada ya kuchinjwa na watu ambao
mpaka sasa hawajajulikana.
Kwa
mujibu wa majirani tukio hilo limetokea katika mkesha wa mwaka mpya
majira ya saa moja usiku, nyumbani kwake maeneo ya Ulowa no 4 ambapo
kikongwe huyo alikuwa anaishi na mtoto wake wa kiume.
Wameeleza kuwa Wakati tukio hilo likitokea, mtoto wake wa kiume ambaye hakutajwa jina lake (miaka 34-40) alikuwa ameenda kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya akiwa na mkewe maeneo ya Ulowa no 5, na wote walirudi nyumbani majira ya saa 10 na usiku ndipo walikuta mwili wa marehemu Milembe Jengamalulu.
Baada
ya kuukuta mwili huo ukiwa nje ya nyumba huku ukiwa umetapakaa damu
nyingi, huku ukionesha kuwa amechijwa kwa kutumia panga na shoka,
walitoa taarifa kwa majirani ambao walisaidia kutoa taarifa kwa uongozi.
Kuuawa kwa kikongwe huyo kunafuatia mfululizo wa matukio mengi ya kuuwawa kwa vikongwe mkoani Shinyanga ambayo yanasadikiwa kuwa yanatokana na Imani za Kishirikina.
Post a Comment