Mpishi:
Lionel Messi (kulia) akishangilia baada ya kumsetia Cristian Tello
(katikati) kufunga hat trick katika ushindi wa Barcelona wa 4-1 dhidi ya
Levante
Furaha pale pale: Lionel Messi akiwapigia makofi mashabiki baada ya kucheza kwa mafanikio mechi ya 400 FC Barcelona usiku huu
*******
TIMU ya Barcelona imemaliza hasira zake za sare ya Jumapili na Levante kwa kuifumua timu hiyo mabao 4-1 usiku huu kwenye Robo Fainali ya kwanza ya Kombe la Mfalme Uwanja wa Ciutat de Valencia.
Mkali wa mabao wa Barca, Lionel Messi amecheza mechi ya 400 katika timu hiyo Katalunya usiku huu, ambazo ndani yake ameshinda mataji sita ya La Liga na matatu ya Ligi ya Mabingwa.
Messi alifanya kazi nzuri akitoa mchango kwa mabao yote manne, ikiwemo hat-trick ya Cristian Tello. Wenyeji walitangulia kupata bao lililofungwa na mchezaji wa zamani wa Liverpool, Nabil El Zhar.
Juanfran alijibabatiza mpira uliopigwa na Messi na akaudondoshea kwenye nyavu zake mwenyewe kuisawazishia Barca- kabla ya Tello kufunga mara tatu mfululizo kuipa ushindi mtamu timu yake.

Credit: Bin Zubeiry blog
on Thursday, January 23, 2014
Post a Comment